Header Ads Widget

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA KIKATIBA YA MBATIA

 



Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia ya kupinga utaratibu wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.


Uamuzi huo umetolewa leo Januari 28, 2022 na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji John Mgeta ambapo amesema kuwa, Ndugai alifuata taratibu zote za kujiuzulu ikiwemo kuandika barua kwa mkono ya kujiuzulu kwenda kwa katibu wa Bunge.


Katika uamuzi huo, mahakama imesema mbali na barua hiyo ya kwenda kwa Katibu wa bunge Ndugai aliwasilisha barua ya pili kwa chama chake kupitia Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ndio kimempa ridhaa ya kugombea nafasi hiyo.


Jaji Mgeta amesema hakuna Mtanzania aliyeiona barua ya Spika kujiuzulu bali iliyokuwa ikisambaa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na chama chake na si barua ya kujiuzulu.


Baada ya kueleza hayo, Jaji Mgeta akampatia Mbatia nakala kivuli(Copy) ya barua ya Ndugai alivyojiuzulu.


Hata hivyo, Mawakili wa Mbatia wamesema kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI