Header Ads Widget

MBUNGE SHEKILINDI AOMBA SERIKALI KUPANDISHI HADHI MJI WA LUSHOTO

Mbunge wa jimbo la Lushoto Mhe. Shabani Shekilindi ameiomba Serikali kuipa hadhi mji mdogo wa Lushoto ili uweze kuingiza vyanzo vyake vya mapato.Mwandishi Ibrahim Kunoga MDTV  Tanga

Ameyasema hayo kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa RCC kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa Mkoa.

Mamlaka ya mji wa lushoto imeanzishwa zaidi ya miaka kumi iliyopita lakini toka kuanzishwa kwake haijapewa mamlaka ya kukusanya mapato.

Mh Shekilindi amesema ni kweli walikaa kikao na kukubaliana mamlaka ile iendelee lakini bado kuna changamoto na kumtaka mkuu wa mkoa atoe baraka zake kwenye kikao cha RCC.

"Wataalamu wakae waende wakagawe maeneo ya mamlaka ya mji ili yapatikane maeneo ya kukusanya mapato vinginevyo mh mwenyekiti hakuna kitakachofanyika;Amebainisha Mh Shekilindi.

Ameongeza kuwa baada ya kupata mwenyekiti mpya ambae ndie mwenyekiti wa halmashauri walikubaliana kwamba mamlaka hiyo ikae na igawe mapato yake lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika na siku zinaenda huku akiomba kikao hicho kitoe maelekezo ili mamlaka ya mji wa lushoto iweze kuendelea na maeneo yao na kukusanya mapato.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI