Header Ads Widget

DC KAYANDA ATOA RAI KWA WAZALISHAJI MBEGU ZA MPUNGA NCHINI


 Mkuu wa Wilaya ya Moshi Abas Kayanda amewataka wazalishaji wa mbegu za mpunga Nchi kuhakikisha kuwa wanazalisha mbegu Bora ambazo zitamsaidia mkulima kuingia katika kilimo Cha kibiashara .

Amesema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya wazalishaji wa mbegu Bora za mpunga  yaliyofanyika katika  chuo Cha  mafunzo ya kilimo moshi (K A T C.) Mkoani Kilimanjaro.

Aidha amesema kuwa kutokana na soko lililopo imeonekana Kuna uhitaji mkubwa wa mbegu za mpunga na Serikali inahimiza wakulima kulima kilimo Cha biashara na sio kilimo cha kujikimu .



"Kwa hiyo nyie ndio mtakaotusaidia kuleta mabadiliko tuliyoyatazamia ,kwani mafunzo haya yatakuwa na faraja Kama yataleta matokeo mazuri na mkizalisha mbegu Bora , mwisho wa siku wakulima wakaona mabadiliko ya mbegu hizo sisi Kama Serikali tunaona faraja ,tumepeleka watu mafunzo na tumeanza kuona matunda yake."Alisema Kayanda.


Hata hivyo amewataka wazalishaji hao kutochakachua mbegu wanazozizalisha kwa kuchanganya na mbegu ambazo sio sahihi  bali wahakikishe kuwa kile walichokizalisha wapeleke sokoni zikiwa bora.


Hata hivyo amesema kuwa wakulima wamekuwa wakianda mashamba lakini anapokosea kupanda mbegu Bora anapataa mazao yasiyoeleweka .



Akizungumza katika mafunzo hayo mratibu wa mafunzo hayo Martin Ndomondo ambaye ni mtafiti wa mbegu kutoka shirika la kimataifa la utafiti wa mpunga ( IRRI )amesema kuwa shirika hilo linafanya shughuli zote zinazohusiana na utafiti wa kilimo Cha mpunga wenye kulenga tija ya uzalishaji wa zao la mpunga na kuinua maisha Ya wakulima wa zao hilo.


Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo maelfu ya wakulima wameweza kupatiwa mafunzo ya moja kwa moja na kusema wanaendele kutoa elimu .


Ameendelea kusema kuwa Lengo la kutoa mafunzo hayo ni kutokana na kuwepo kwa ukosefu wa mbegu Bora za mpunga ukilinganisha na mazao mengine ambapo amesema kuwa mbegu hizo za mpunga zimeonekana kutokuwa na soko zuri .


"Hii imekuwa ikichangia  kushuka kwa tija ya uzalishaji wa mpunga ,tafiti zilizofanywa na taasisi za Kiserikali na za kimataifa zimeonesha kwamba chini ya 10% ya wakulima Tanzania pekee ndio wanaotumia mbegu Bora .


Amesema kuwa kiasi Cha mavuno ambayo yanapatika kwa wastani wa wakulima kwa nchi ni chini ya Tani mbili kwa hekta na sababu kubwa ni kutokutumia mbegu bora.


Hata hivyo amesema  kuwa Wanashirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa mafunzo hayo  ambapo wadau hao  ni pamoja na  Taasisi ya utafiti wa mbegu Tari, Shirika la uthibiti wa mifumo ya mbegu Tanzania Toski, Wakala wa mbegu Tanzania ASA, Asasi isiyo ya Kiserikali ya Kilimo Trust.


Nao wakulima walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa ni mazuri kwani yamewafunzo hayo wamesema kuwa wwamepata elimu ambayo wataenda kuyafanyia kazi ili kuleta faida na tija katika uzalishaji wa mbegu Bora za mpunga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI