Header Ads Widget

MANISPAA YA MOSHI YAFICHUA SIRI YA KUPEWA TUZO YA USAFI WA MAZINGIRA

 



Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Rashid Gembe amefichua Siri ya kupata tunzo ya usafi wa mazingira kuwa ni ushirikiano uliopo kati yao na  madiwani, watumishi pamoja na kufuata Sheria walizojiwekea wenyewe.


Amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema kuwa ushirikiano ndio chanzo Cha kuibuka na tuzo  usafi wa mazingira.


"Vile vile tunajitahidi kuhakikisha kwamba magari yetu tuliyonayo yanazoa taka kwa haraka na pia zinapokuwa na hitilafu tunazitengeneza kwa wakati ili kuepuka ucheleweshwaji wa uzoaji wa takataka"Alisema Gembe.


Hata hivyo amewataka wananchi wa Moshi kuendelea kuwa wasafi ,na kufuata Sheria walizojiwekea ili mji wa Moshi uendeelee kuwa msafi.


Kwa upande wake msatahiki meya wa manispaa ya Moshi Mh.Juma Raibu amesema kuwa mwaka 2021/2022 walipewa tuzo ya usafi wa mazingira Taifa kwa maana ya halmashauri ya wilaya Moshi kuongoza kwa usafi Tanzania mzima.



"Katika halmashauri za manispaa zote za nchi hii zaidi ya ishirini sisi tuliongoza  lakini kwa ujumla tuna halmashauri 184 lakini sisi halmashauri ya wilaya ya Moshi tumekuwa wa kwa kushinda usafi"Alisema Raibu.


Katika hatua nyingine amesema kuwa Katika ushindi huo wamepewa zawadi ya hundi ya milioni 20 na kombe na cheti Cha usafi wa mazingira kupitia aliyekuwa waziri wa Afya Dr Dorothy Gwajima.


Hata hivyo amewataka wananchi kuhakikisha kuwa hawatupi taka taka hovyo kwani yeyote atakauegundulika atatozwa faili ya sh.Elfu Hamsini bila kuangalia kuwa yeye ni nani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI