Jumla ya kaya 42 zilizopo Mtaa wa Kineng'ene Kata ya Mtanda halmashauri ya Lindi zimekosa makaazi baada ya nyumba zao kuezuliwa kufuatia Mvua iliyoambatana na upepe Mkali iliyonyesha juzi na kuharibu makazi yao...............NA..HADIJA OMARY
Katika kata ya Mtanda mtaa wa kineng'ene Manispaa ya Lindi Mkoani humo umesababisha Athari kwa kaya 42 nyumba zao kuezuliwa pamoja na majengo Mawali ya Umma.
AKitoa taarifa juu ya Athari iliyotokana na mvua hiyo kaimu mtendaji wa kata ya Mtanda Salum Jumbe alisema kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepe mkali ilianza majira ya saa sita na dakika 45 mpaka saa saba kamili mchana na kusababusha athari kwa baadhi ya Wananchi pamoja na majengo mawili ya Umma
Alisema taarifa hiyo ya kaya 42 ni ya awali hivyo idada hiyo inaweza kuongezeka baada ya kuendelea kukusanya taarifa kutoka kwenye vitongoji huku akitaja Majengo ya Umma yaliyoathilika kuwa ni kituo Cha Afya kineng'ene pamoja na ghara la kuifadhia Mazao
"Athari zilizotokea kwenye majengo ya Umma hasa kwenye kituo cha afya pia ni kubwa ambayo imehusisha chumba cha Chanjo, Ukumbi wa RCH na chumba chake, Wodi ya Wanaume, Store kubwa ya Dawa, Duka la Dawa, pamoja na store ya Gesi, "
"Kwa upande wa majengo mapya ya kituo hiko cha afya athari zilizojitokeza ni pamoja na Mlango wa chumba cha kujifungulia akina Mama wajawazito, Nyumba ya muhudumu wa kituo kuezuriwa upande wa choo pamoja na fisha bodi kuezuriwa huku Gara la kuifadhia mazao kezuliwa paa lote" alisema Jumbe
Kufuatia hali hiyo Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Hamida Abdallah alifika kutoa pole kwa Waathirika wa Mahafa hayo kwa kuwapatia Unga wa sembe viloba 42 vya kilogram 25 pamoja na Maharage kilogram 210 ambavyo kila kaya iliyoathirika itapatiwa kiroba kimoja cha Unga na maharagwe kilogram 5 pamoja na kuhaidi kuchangia shilingi milioni 1 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la kituo cha Afya
"Wakati serikali inaendelea na zoezi la kuchukua takwimu na idadi ya Wahanga walioathilika na tukio hili nikaona sio vibaya nikaja kuwasalimia, kutoa pole na kuwapa kidogo nilichonacho, tunajua baada ya kuezuriwa majumba Chakula kimelowa ndani ya Nyumba kwa hivyo inawezekana mtu akakosa kula ugali au hata uji kwa Watoto hivyo hii ni hatua ya mwanzo kwangu na serikali ya Wilaya itakuja hapo baadae" alisema Hamida
Wakizungumza kwa masikitiko kwa niaba ya wanzao Fatuma Minduva, Rukia Kunguru walisema kuwa mvua hiyo pamoja na kuaribu Nyumba zao lakini pia vitu vilivyokuwepo humo kuloa na maji ikiwa pamoja na Magodoro, Nguo, madafutali ya Wanafunzi na hata Akiba yao ya chakula hivyo pamoja na mbunge kutoa msaada huo bado wanahitaji msaada kutoka kwa wadau wengine
"Namshukuru mheshimiwa Mbunge kwa Msaada aliotupatia kwani mimi Wakati ule mvua inaanza kunyesha nilikuwa msikitini baada ya kurejea nyumbani nikakuta nyumba yangu imeezuliwa Bati vitu vyangu vyote vimeloa sikujua hata nianzie wapi hivyo kwa msaada huu angalau nimepata chakula na watoto nyumbani " alieleza Fatuma Minduva
Akitoa salam za Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga afisa Tarafa wa Wilaya hiyo sharifa Mkwango aliwasihi waathirika hao kuendelea kuwa wavumilivu wakati Serikali ya Wilaya inaendelea kufanya utaratibu wa Namna ya kuwasaidia
0 Comments