WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewaagiza Makatibu wakuu kushirikiana na Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) kutafuta namna nzuri ya kuwaandaa wastaafu mapema kabla ya kustaafu kwao .
Mhagama ametoa agizo hilo jijini hapa kwenye kikao cha kujadili Tathmini ya utekelezaji wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge sera kazi ajira na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo amewaagiza wenye mifuko ya hifadhi ya watumishi inayofanya mafunzo hayo kutengeneza mpango utakaoweza kuwaandaa wastaafu watarajiwa kisaikolojia.
“Najua hatuwezi kufanya mafuzo kila siku lakini angalau tutengeneze makundi..ili wajue wakati labda wamebakiza miaka kumi kabla kustaafu ili waweze uanza biashara kwakuwa hauanzi kuannza biashara leo kesho ikakuwa,”amesema
Amesema hata biashara kukuwa kama anavyotunzwa mtoto kwa kuwekeza sehemu fulani muda muda mrefu ambapo baada ya kuwekeza fedha ya kustaafu kwenye biashara hiyo ndio huleta matokeo chanya ya fedha za kustaafu.
“ni ukweli yani mtu anakaribia miezi mitatu kustaafu alafu PSSSF mnamwambia habari ya kujiandaa na maisha kinachoweza kutokea hapo inaweza kuwa ni habari nyingine ama anaweza kuwekeza fedha yake mahali ambapo sio sahihi," amesema
Na kuongeza" Sasa PSSSF muangalie namna bora ya kutoa na kuandaa mafunzo ili wastaafu wapate muda wa kutosha wa kupima wanayoshauriwa kwenye mafunzo hayo kama kweli wanaweza kuyatekeleza ili siku ya mwisho wapate elimu ya kitu kitakachoweza kuwasaidia.
Akizungumzia suala hilo Naibu Katibu Mkuu kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Profesa Jamal Adam Katundu amesema kwenda kwenye mafunzo ya kustaafu ikiwa imebaki muda mchache inawachanganya watumishi hao.
“Kumpa mtu mafunzo ya kustaafu ikiwa imebaki miezi sita ni kumchanganya tu lakini tukijipanga kwa kuangalia tuna watu hawa watastaafu ndani ya miaka mitano kustaafu na ikiwa kuna uwezekano tuangalie namna ya kuwawekea bajeti na kama tukiwa tunaenda nao hivi akibakiza mwaka mmoja kamradi kake kakuku kashaanza kusimama” amesema
Naye Mwenyekiti waShirikisho la vyama vya wafanyakazi TUGHE kutoka Ofisi ya Waziri mkuu Numpe Mwambenja alimuomba Jenista kuwezesha watumishi kwenye upandishwaji wa madaraja, uwezeshwaji wa watumishi wanapopatwa na changamoto za kiafya na misiba pamoja na mafunzo mbalimbali ya watumishi kulingana na kada zao.
Kwa upande wao Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wameiomba Serikali kutoa utaratibu wa kupewa mafunzo kwa wastaafu watarajiwa yanayotolewa muda mfupi kabla ya kustaafu wakisema huwapa presha.
Akiongea kwa niaba ya wenzake mmoja wa wafanyakazi waliohudhuria kikao hicho amesema suala la kuwapa wastaafu watarajiwa mafunzo ya muda mfupi kabla ya kustaafu ni kuwachanganya kisaikolojia kwakuwa wengi hutamani kujaribu kila wanachoelekezwa na kujikuta wanamaliza fedha zao bila mafanikio .
“Bila kujali una miaka 15 au 20 ya kustaafu, Naomba Mheshimiwa Waziri haya mafunzo yawe ya mara kwa mara kwenye Taasisi zetu ili iwe kumbusho la wapi tunapoelekea ," amesema …
kwasababu tumeshaona wastaafu wengi wanafanyiwa mafunzo yale kwenye dakika za mwisho,, anatoka kutembezwa kwenye miradi lakini amebakisha miezi sita unadhani itamsaidia nini” alisema mmoja wa watumishi hao.
0 Comments