Header Ads Widget

BODABODA ULANGA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

 



Wito umetolea kwa waendesha bodaboda katika Wilaya ya Ulanga kwa kufuata sheria za usalama barabarani na  kuhakikisha wanaziepuka ajali za uzembe nakumfikisha salama abiria anayetumia usafiri huo 



Wito huo umetolewa na wajumbe kamati ya usalama barabarani wilaya ya ulanga wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyozinduliwa katika kijiwe cha bodaboda kilichopo Togo Mahenge Wilayani Ulanga 



Wajumbe hao wamesema kuwa endapo kila mwendesha bodaboda atazingatia na kufuata sheria za barabarani hakutakuwa na ajali katika mji wa mahenge na wilaya kwa ujumla wake hivyo wamewataka bodaboda hao kuzingatia sheria zote za barabarani 




Kwa upande wake mkuu wa usalama barabarani JOSEPH SAGALA amesema kuwa kwa mwaka huu wiki ya nenda ka usalama itafanyika kwa kuwatembelea bodaboda kwenye vituo vyao na kuwapatia elimu ya uslama barabarani ili wasio jua sheria wazijue ili kutokomeza ajali za uzembe 



Mkuu huyo wa usalama barabarani  amesema kuwa wameandaa vyeti vya Madereva bora kwa mwaka huu na watapatiwa vyeti wale madereva wote ambao hajawahi kupata ajali wakati wote wa kazi yao ya bodaboda 



Aidha mkuu wa polisi wilayani ulanga JAKSON KAHAMBA  amesema ili kutokomeza ajali wilayani ulanga amewataka bodaboda kufika ofisini kwake mara tu wanapoonewa na askari wa usalama barabarani kwani kwa kuhofia kusema ukweli itawapelekea kuzidi kuonewa nayeye asiwe na taarifa ya kuonewa kwao



Mkuu wa Polisi amesema kuwa anasikitishwa na baadhi ya Madereva wa  bodaboda ambao wanaonekana kuonewa na hawasemi wanasubiri mpaka kuwe jna mkutano wa hadhara jambo ambalo hajapendezwa nalo



Akihitimisha uzinduzi huo Mwenyekiti wa kamati ya nenda kwa usalama Wilayani Ulanga Bw Christom Msakamba amewataka vijana kuhakikisha ulanga inakuwa haina ajali kwa kufuata sheria za barabarani 



Nao bodaboda wameomba uongozi huo kuwapa mafunzo ya mara kwa mara na kusaidia  kuwapatia leseni kwa bei nafuu,pamoja na kuahidi kupokea yale waliyopewa na kuyafanyia kazi ili kutokomeza ajali za barabarani za uzembe 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI