MABINGWA wa tetezi wa soka mkoa wa Pwani timu ya Nyika FC ya Kibaha imefanikiwa kutetea ubingwa huo baada ya kuifunga timu ya Kerege ya Wilaya ya Bagamoyo bao 2-0. mwandishi wa matukio daima John Gagarini anaripoti kutokea Pwani
Timu hizo zilikutana kwenye hatua ya fainali mchezo uliopigwa uwanja wa Dawindege Kilindoni wilayani Mafia.
Kufuatia ushindi huo Nyika FC watacheza na Mabingwa kutoka katika Mikoa mingine kwenye michuano ya RCL .
Kwa ushindi huo Nyika FC watacheza Ligi Daraja la tatu huku michuano hiyo ikiwa imeandaliwa na Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA).





0 Comments