Imeelezwa kuwa kilimo cha ikolojia endelevu ni kilimo kinachozingatia upatikanaji wa lishe bora pamoja na kutunza mazingira kwa ajili ya kilimo endelevu. mwandishi wa matukio daima Namnyak Kivuyo anaripoti kutokea Arusha
Hayo yalielezwa na Afisa mradi wa mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA) Damian James Sulumo katika mafunzo waliyoyatoa kwa waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na kilimo endelevu kwa kutumia mbegu za asili ambapo alisema kuwa kuna faida nyingi katika kilimo cha kiiolojia kwani kinaweza kusaidia kulisha Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Alisema kuwa serikali inapaswa kuwajibika kwa kutambua umuhimu wa mbegu za asili kwenye sheria kwani ni mbegu ambazo wakulima kwa asilimia 80 wanazitumia katika kufanya uzalishaji lakini pia serikali ibadilishe mtazamo na kuwafundisha maafisa ugani kuwa kilimo cha kiiolojia kinaweza kutunza mazingira.
Alifafanua kuwa mfumo wa kilimo endelevu ni mfumo ambao unatoa usalama wa chakula na lishe kwa wote kwa njia ambayo misingi ya kiuchumi, kijamii na kimazingira inazingatiwa kwa vizazi vyote ambapo pia aliiomba serikali na wadau wengeine kuupa kipaumbele mfumo huo ili kuwa na chakula Cha kutosha na lishe kamili.
“Ni muhimu kufuata mambo ambayo yanatupeleka katika mfumo wa kiiolojia kama njia ya kuelekea mifumo endelevu ya chakula ambayo ni njia jumuishi inayotumia dhana ambazo aziathiri mazingira lakini pia kuimarisha uhuru wa mkulima na nguvu ya mkulima,” Alisema Damian.
Kwa upande wake Abdallah Mkindi mwezeshaji kutoka mtandao wa Bioanuai Tanzania (TABIO) alisema kuwa Kuna aina mbili za mbegu ambazo ni mfumo rasmi wa mbegu ambazo ni zile zilizifanywa isibati na mfumo wa mbegu usio rasmi ambao ni mbegu za wakulima ambapo mfumo huo inachangia upatikanaji wa mbegu kwa asilimia 90.
“Mfumo huu wa mbegu za wakulima ni mbegu ambazo hazifanyiwi isibati na uzalishaji wake ni sehemu ya uzalishaji wa chakula na mkulima ndiye anayemiliki mbegu na wanagawiana au kuuziana wao kwa wao lakini sheria inapinga mfumo huu hali inayomnyima mkulima haki ya kusambaza mbegu za asili anazozizalisha,”Alisema Mkindi.
Mwakilishi kutoka mkulima mbunifu Flora Laanyuni aliwataka wanahabari kutumia kalamu zao kupaza sauti za wakulima na ubora wa mbegu za asili katika taarifa zao ili kuweza kuleta suluhu katika changamoto zinazowakabili na kuwafanya watoke hatua moja kwenda nyingine.
“Tuandike makala zitakazotoa fursa kwa wakulima kujifunza vitu vipya na zitakazo jibu mahitaji ya kilimo na hii itakuwa ni njia mojapo ya kumthamini mkulima na kuweza kuielimisha jamii juu ya faida za kutumia mbegu za asili,” Alisema Flora.
0 Comments