Header Ads Widget

MKE WA MCHUNGAJI HUYU AJINYONGA KATIKATI YA SHEREHE ZA KRISMASI

 


NAATUKIO DAIMA MEDIA RUKWA 

MKE wa mchungaji wa kanisa la EAGT kijiji cha Kanazi Rukwa Joyce Baton Mwasumbi mkazi wa Kijiji cha Kanazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kanga chumbani kwake.

Akizungumza na Matukio Daima Media juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kanazi Rudis Ulaya amesema kuwa tukio la Mwanamke huyo ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT katika kijiji cha Kanazi kujinyonga limetokea leo Jumatano Disemba 24,2025 majira ya saa 2 asubuhi baada ya Mumewe ambaye ni mchungaji kwenda kanisani kupalilia pembeni mwa jengo la kanisa hilo.

Amesema kuwa wakati Mumewe ambaye ni Mchungaji akiendelea na jukumu lake kanisani mkewe aliutumia mwanya huo kujitundika kwa kutumia kitenge na muda mfupi Mumewe aliingia chumbani huko na kumkuta Mkewe akiwa amejitundika juu huku akitapatapa kufa ndipo alipochukua kisu na kukikata kitenge hicho kwa lengo la kuokoa uhai wake lakini muda mfupi alipoteza maisha


Mwenyekiti huyo wa Kijiji amefafanua kuwa baada ya yeye kumhoji Mume wa marehemu Mchungaji Ibrahimu Mwaipopo alidai kuwa huenda kifo Cha mkewe kimetokana na deni alilokuwa nalo ambapo alikopa fedha za kanisa hilo na siku za hivi karibuni alionyesha kukosa furaha kutokana na deni hilo na kuwa huenda jambo hilo likapelekea Mwanamke huyo kujinyonga.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Shadrack Masija amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini chanzo halisi kilichopelekea Mwanamke huyo kuchukua uamuzi huo mzito wa kujinyonga.

Pia ameishauri jamii kushirikisha Watu pale wanapokumbwa na changamoto mbalimbali badala ya kuchukua maamuzi magumu kama hayo ya kujitoa uhai

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI