Header Ads Widget

URU FUN MARATHON YAFANA MOSHI




Matukio Daima, Moshi

MKUU wa wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava ameongoza wakimbiaji zaidi ya 400 kushiriki mbio za Uru Fun Marathon zilizoanzia eneo la Uru Mingeni, Kata ya Uru Kusini.

Tukio hilo lilmeambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Anieli Foundation inayojikita katika huduma za elimu, afya na mazingira bila malipo huku kwenye afya magonjwa wakiangazia zaidi yale yasiyoambukiza na yasiyopewa kipaumbele yanayoweza kudhibitiwa zaidi kwa mazoezi ikiwemo Shinikizo la damu na kisukari.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, ndiye aliyeogoza mbio hizo na  kuzindua rasmi taasisi hiyo iliyobuniwa kwa kumbukizi ya marehemu Elizabeth Michael Mushi na mumewe Anizeth Mushi, alisisitiza umuhimu wa wananchi kufanya mazoezi kama kinga ya magonjwa yasiyoambukiza.

 

“Mazoezi ni tiba, na ni lazima yawe sehemu ya maisha yetu, si kusubiri mashindano,” alisema mkuu huyo wa Wilaya.

Huduma za afya zilizotolewa Kwa mara ya kwanza na taasisi hiyo ni pamoja na upimaji wa kisukari, shinikizo la damu, uzito na uchangiaji damu Kwa hiyari chini ya usimamizi wa madaktari kutoka Hospitali ya Mawenzi na KCMC kupitia kaulimbiu “Afya Yako Mtaaji Wako.”


Mwenyekiti wa Anieli Foundation, Gaudence Mushi, alisema taasisi hiyo inalenga kuisaidia jamii kiafya, kielimu na kimazingira kwa kuanzia na Uru Kusini kabla ya kupanua huduma maeneo mengine na shughuli hizo zitafanyika kila Oktoba 03 kila mwaka, siku aliyofariki bi Elizabeth.


Dkt. Phillip Makupa alionya kuongezeka kwa magonjwa kama shinikizo la damu na kisukari, akisema sasa yanawakumba hata vijana wadogo kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, akishauri mazoezi, ulaji bora na kupima mara kwa mara wa afya.


Mratibu wa mashindano hayo, Adv. Wilhad Kitali, alisema marathon hiyo ni msimu wa pili na inalenga kujenga utamaduni wa mazoezi kwa jamii, huku washindi wakikabidhiwa medali na zawadi za fedha taslimu kwa makundi mbalimbali.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI