Picha ya mtandaoni haihusiani na habari hii
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Makete mkoa wa Njombe imemhukumu mwanafunzi wa shule ya msingi Lupalilo (13) kwenda jela miezi sita na kulipa Faini 8500 kwa makosa ya wizi wa vitu mbalimbali, imetolewa
Huku Anna Sanga (36) wa kijiji cha Lupalilo wilayani aliyeshitakiwa pamoja na mwanafunzi huyo akiachiwa huru .
Washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo Septemba 4, 2021 majira ya saa 5 asubuhi huku mlalamikaji akiwa Sara Sanga (50) ambae alidai kuibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki 8 na elfu 85 ambavyo ni mali yake halali
Hata hivyo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wake dhidi ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Anna Sanga baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani pasipo shaka
Mahakama hiyo imemhukumu mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Lupalilo kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya shilingi 85,000 kwa mlalamikaji
Hukumu hiyo imetolewa Novemba 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki pamoja na mwendesha mashtaka wa serikali Asifiwe Asajile.
Chanzo;Greenfm radio Makete
0 Comments