Alisema vitendo hivyo ambavyo vinaendelea kushamiri hapa Zanzibar huathiri vijana ambao ndio tegemeo la taifa la kesho .
Aliyasema hayo katika mafunzo ya haki za binaadamu na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe, ambayo yaliwashirikisha wanafunzi mbali mbali kutoka shule za msingi na sekondari zilizopo wilaya ya magharibi A na B.
Aidha alisema jumla ya kesi 868 zimeripotiwa kwa mwaka huu ambapo kesi 567 ni za watoto wa kike sawa na asilimia 68 jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya taifa.
Kamishna huyo amewataka wanafunzi hao kueleza matatizo mbali mbali wanayokumbana nayo katika jamii ili kutafutiwa ufumbuzi muafaka kupitia tume hiyo kwa lengo la kuzishauri serikali zote mbili kutokana na changamoto hizo zinazojitokeza.
Kwa upande wa wanafunzi hao walisema uelewa mdogo wa wazazi na walezi katika jamii kuhusu vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia unapelekea vitendo hivyo kuzidi kuongezeka.
Walisema kutokana na umasikini, hali duni ya maisha ,mporomoko wa maadili kwa kuziacha mila, desturi na tamaduni za awali pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii huchangia kuwa na tamaa kwa wanafunzi na hupelekea kufuata ushawishi na ulaghai ambao huchangia vitendo hivyo.
Nao Wanafunzi hao walitoa wito kwa wazazi na walenzi kuwa karibu na watoto wao kwa kuwapa ushauri na mbinu za kuepukana na vitendo hivyo vinavyowapotezea ndoto zao .
0 Comments