Zaidi ya Tani 4000 za Korosho ghafi za wakulima wa Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale zimeuzwa kwenye Mnada wa pili wa Chama hiko kwa bei ya juu ya shilingi 2'311/= na bei ya chini shilingi 2'240/=kwa kilo. mwandishi wa matukio daima Hadija Omary anaripoti kutokea Lindi.
Mnada huo umefanyika leo katika kijiji cha Makanjilo kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo jumla ya Makampuni 14 yalijitokeza kuomba kununua korosho hizo huku makampuni manne pekee ndio yaliyoshinda kwenye mnada huo.
Katika Mnada huo Ghala la Expot Nachingwea limeingiza jumla ya kg 427,613, Ghala la lindi farmers Nachingwea kgs 287'742, Ghala la Nachingwea DC kgs 673'067, Ghala la Umoja liwale kgs 1'314'987, na Ghala la Lipande Ruangwa kgs 1'602'652.
Akizungumza na wakulima walioudhuria Mnada huo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrew Chikondwe aliwahasa Wakulima wa chama hicho kuzingatia ubora wa korosho zao pindi wanapopeleka kwenye maghala ili kuweza kupata bei mzuri.
Nae mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI Odasi Mpunga alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto za Bei zilizopo hivi sasa ni vyema Serikali ikajikita katika kuwekeza katika viwanda vya ndani vya ubanguaji wa korosho uwenda ikawa na tija kubwa kwa wakulima kuliko uuzwaji wa sasa wa korosho ghafi .
Kwa upande wao Baadhi ya wakulima walioshiriki katika Mnada huo walisema kuwa pamoja na kwamba wamekubali kuuza korosho zao bado bei zilizopo sokoni sio rafiki kwao ukilinganisha na nguvu walizotumia katika kuhudumia mashamaba yao.
0 Comments