Header Ads Widget

WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

 

_Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

 January Y. Makamba (Mb), Waziri wa Nishati amewasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

 

Mheshimiwa Makamba amewasilisha ujumbe huo maalum kupitia kwa Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje,  tarehe 24 Oktoba, 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE. 

 

Mheshimiwa Makamba yupo Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Mafuta na Gesi. 

 

Mheshimiwa Makamba katika mazungumzo hayo ameambatana na Mhe. Mohamed Mtonga, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Kamishina wa Mafuta na Gesi, Ndg. Michale Mjinja kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI