Header Ads Widget

TOZO YA MIAMALA KUWAFUTA MACHOZI AKINA MAMA MTAMA

 



Na Hadija Omary _Lindi


Ikiwa leo ni oktoba 15 ambapo Mataifa yote ulimwenguni yakiadhimisha siku wanawake vijijini , Wanawake wa kata ya Mtama Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya katika kata yao.


Wakizungumza na Matukio Daima  Wanawake hao  walisema kuwa ujenzi huo wa kituo hiko cha Afya utaenda kupanua huduma za uzazi pamoja na huduma zingine walizokuwa wakizipata kutoka katika zahanati pamoja na kupunguza gharama ya kusafiri kwenda Hospital ya Nyangao kwa ajili ya kupata huduma 


Nae Melina kambona Mkazi wa Mtama  alisema kuwa kwa sasa wananchi hao wanapata huduma katika ngazi ya zahanati  ambapo kulingana na wingi wa wagonjwa wanaoenda kupata huduma katika zahanati hiyo ulazimika kuchukuwa muda mrefu kusubiri huduma na pengine kwenda hospitali ya nyangao kupata huduma zingine ambazo kwenye zahanati hiyo haipatikani




Alisema uchache wa vifaa na wahuduma ukilinganisha na wagonjwa wanaofika katika zahanati hiyo pia ni changamoto kwani wakati mwingine mpaka mama anaweza kujifungua nje kabla ya kuanza kupatiwa huduma


"Kwa mfano sasa hivi mjamzito uchungu ukimuanza anapelekwa zahanati unaweza ukakuta wajawazito wengine wako pale wanapata huduma na vile madaktari walivyokuwa kidogo kwa hivyo nuss anajitahidi kadili ya uwezo wake ili kumsaidia ila lakini utakuta mama yule anajifungulia pale pale nje kabla hajaingia ndani kutokana na uhaba wa vifaa" alifafanua


Nae Fatuma seleman  alisema kuwa kituo hiko kitakapokamilika kitawawezesha kupata huduma za uzazi kwa urahisi hivyo anamshukuru Rais Samia kwa kutoa kiasi hiko cha fedha kwa ajili ya ujezi wa kituo cha Afya


" Tunamshukuru sana mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kutusogezea huduma hii karibu kwani sasa tutakwenda kupata huduma ya uhakika hata upasuaji wa uzazi tupata hapa" alisema fatuma


Nae Salum Chande alisema Kutokana na kokosa kwa baadhi ya huduma katika zahanati hizo akinamama walikuwa wakisafiri kwenda Hospital ya nyangao jambo ambalo ilikuwa usumbufu na pengine kupelekea mpaka kifo kwa mama mjamzito akiwa njiani kuelekea Hospital. 




Kwa upande  wake Abruhami juma  Mhadisi wa ujenzi Halmashauri ya Mtama alisema fedha za Mradi huo zimetokana na makato ya miamala ya simu ambapo kwa awamu ya   kwanza  utahusisha Majengo ya mahabara, kichomea taka pamoja na jengo la wagonjwa wa nje  na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Desemba mwaka huu.


Hata hivyo aliongeza kuwa mara baada ya Kukamilika kwa Mradi huo wa kituo cha Afya  Wananchi wa Mtama wataweza kupata huduma za  X_Rey, Jengo la Uzazi na Mahabara ambozo katika Zahanati waliyokuwa wanapata huduma hazikuwepo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI