Familia na marafiki wa wapendanao hawafichi furaha yao walipohudhuria sherehe ya kimila ya harusi iliyofanyika Oktoba 9 mwaka 2021.
Katika harusi hiyo ya Bibi harusi Erumena, kulikuwa na msururu wa wapambe na wasindikizaji wa binti harusi 'maids' ambao ni marafiki zake wa muda mrefu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ambao bibi harusi anawaita ' wasaidizi wa heshima'
Marafiki zake hao wa muda mrefu na urafiki wao ulidumu kwa muda mrefu wengi wao wanaitwa sasa bibi, maprofesa na mama, kutokana na umri wao kusonga.
Mmoja wa wasaidizi hao alilazimika kusaifiri kutoka London kuja kushuhudia harusi hiyo ya kihistoria.
Kwanini kachelewa kuolewa?
Bibi harusi huyo ambaye watu hupenda kumuita Anti Mena, ameiambia BBC kwamba mazingira magumu ya kimaadili aliyokulia yamechangia kwa kiasi kikubwa asiweze kuolewa haraka. Miaka ilivyozidi kwenda kuanzia 30, mpaka 40 na baadae 50 kwenda 60 alikua akikumbana na changamoto kadhaa kama kukejeliwa na baadhi ya watu.
"Umezeeka, hufai kuolewa, wewe mrefu unaolewa na mtu mfupi. Wewe ni mzee hata kama ukipata mwanaume, utapata mzee kuliko mie', ni baadhi ya kejeli anazosema Erumena, ambaye anaongeza kuwa hakuruhusu kejeli hizo na nya watu kumtikisa.
Hata marafiki zake, ndugu na wafanyakazi wenzake walioa mmoja baada ya mwingine, lakini bado aliendelea kujumika nao na kufurahia nao pamoja.
"Kila mwaka nilikuwa najisemea ikifika Disemba mwaka huu, nitaenda kuishi na mume (nitaolewa), lakini Disemba inafika na kwenda, sifanikiwi, lakini nashukuru imefikia oktoba 2021, "madam Erumena aliambia BBC.
Erumena siku ya harusi yake
Anti Mena anaongeza kwamba hataki kusubiri changamoto alizopitia peke yake. Changamoto aliyonayo sasa ni kupata mtoto, alitaka kupata mtroto akiwa ndani ya ndoa, na ndoa amshaipata.
Licha ya umri wake, haonyeshi kukata tamaa ya kupata mtoto, anaendelea kuwa imara hadi sasa anapopata mpezi wake wa maisha akiwa na umri wa miaka 64.
Anaongeza kusema sababu nyingine iliyochangia kuchelewa kwake kuingia kwenye ndoa ni kwamba yeye sio "mtoto wa barabarani" , hakupenda kuvamia mtu ilimradi mtu tu, kwa hivyo anaendelea tu kudumisha maadili madhubuti ya maisha.
Alikutanaje na mpenzi wake wa maisha?
Kuhusu jinsi alivyokutana na mumewe, Erumena anasema walikutana na kupitia" rafiki mmoja " aliyewaunganisha.
Kuanzia hapo wawili hao waliendelea na mazungumzo kupitia WhatsApp na kupigiana simu. Uhusiano wao uliendelea kudumu na ukawa na muelekeo mzuri zaidi pale mpenzi wake huyo Benjamini alipomtembelea Port Harcourt anapoishi na baadae ya yeye alienda kumtembelea huko Warri.
Anasema kwa mara ya kwanza alipomtembelea Benjamin huko Warri, kuna kitu kilimwambia; "hapa ni nyumbani kwangu."
Anti Mena anamuelezea mumewe kama mtumishi ambaye ni mpole na muelewa.
Anasema mumewe ni mtu wa mungu na ana hofu ya mungu, na kitu hicho anasema ndicho kilichomfanya avutiwe nae na kumpenda. Anawashauri wanawake wenye umri wa miaka 20, 30, 40 na kuendelea wasikate tamaa, mtu sahihi atajitokeza na wataolewa.
Anasema haipaswi kukimbilia kwenye ndoa ama kujiingia kwenye misukosuko, muhimu ni kupata mtu sahihi na 'usiseme nimechelewa'.
Erumena Amata ameolewa akiwa na miaka 64 na mumewe pasta Benjamin Akpoghene-Adaiah ana miaka 69.CHANZO BBC
0 Comments