Header Ads Widget

MWANAHARAKATI AIFUNGUKIA MAZITO SERIKALI

 Na Mwandishi Wetu.

SERIKALI imeombwa kutoa kipaumbele katika mambo muhimu ikiwemo kutoa huduma za maji,elimu na miundombinu hasa katika maeneo ya pembezoni mwa mji ili kuweza kuwasaidia wananchi kupata huduma za jamii kwa wakati.



Akizungumza  jijini jana Mwanaharakati Huru wa kata ya Kivule Bihimba Mpaya alisema kuwa maeneo ya pembezoni hasa katika kata ya Kivule kumekuwa na changamoto nyingi za huduma za jamii ikiwemo upungufu wa madawati pamoja na majengo ya shule.

Akitolea mfano eneo hilo alisema kata ya Kivule ina shule za msingi tano ambazo ni Kivule,Serengeti,Misitu,Bombambili na Anex.


"Shule  zipo lakini kama hazijakamilika,zina idadi kubwa ya wanafunzi mfano shule ya msingi Serengeti ina wanafunzi  2500,Kivule ina wanafunzi zaidi 4000 lakini bado namba kubwa ya wanafunzi wanakaa chini hawana madawati,mbali na hivyo pia kuna changamoto ya vyoo vya walimu jambo linalosababisha walimu kulazimika kujisaidia  you vilivyopo katika nyumba za jirani karibu na shuleni,"alisema Mpaya.


Akizungumzia changamoto ya barabara za mitaa katika kata hiyo yenye mitaa minne ambayo ni mtaa wa Magole,Kivule,Kerezange na Bombambili.

Alisema barabara  katika kata ya Kivule  zimekuwa hazipitiki hasa kipindi cha mvua.

"Mvua ikinyesha barabara hazipitiki gari haziwezi kwenda mpaka Magole kwa sababu maji yanajaa katika maeneo na yanakaa kwa muda mrefu,"alisema Mpaya.


Alisema pia barabara inayoelekea Zahanati ya Kivule  pamoja  na kusisitiza kuwa miundo mbinu ya ndani ya zahanati hiyo nayo ni changamoto .

Akizungumzia kuhusu maji

anasema nayo ni changamoto  kwakuwa watu wengi wanatumia maji ya visima ambavyo vimechimbwa na watu binafsi.

"Maji watu wanayapata kupitia visima vilivyochimbwa na watu wenye uwezo wa kifedha na kusambaza maji kwa wananchi ambayo wanauza kwa  uniti moja Sh 2,000 mpaka 3,000 fedha ambayo ni kubwa ukilinganisha na maji ya Dawasa,"alisema Mpaya.

Alisema kutokana na changamoto hizo ni vema serikali iwe inangalia vitu hivi muhimu vyakutelekeza kwa wananchi badala yakutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ununuzi wa ndege.

"Huwezi kununua ndege wakati hutoi elimu ya uhakika,wananchi hawana mani,shule hazina madawati tuwe tunatoa vipaumbele katika vitu vya muhimu kwa jamii,"alisema Mpaya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI