Header Ads Widget

JAMII YA KIMASAI YASHAURIWA KUACHA KUWASHAWISHI WATOTO KUFANYA VIBAYA KATIKA MITIHANI YAO ILI WAOLEWE.





 Na Rehema Abraham Kilimanjaro

Wazazi na walezi wa Jamii ya kifugaji (maasai )Wilaya ya Simanjiro mkoani manyara wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwashawishi watoto wao wafanye vibaya katika mitihani ili wapate nafasi ya kuolewa.


Kauli hiyo  mrakimu mwandamizi wa uhamiaji Mbaraka Batenga akiwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa simanjiro Makongoro Nyerere Katika uzinduzi wa kampeni ya NIACHE NISOME iliyozinduliwa na shirika lisilo la kiserikali la Elimisha Simanjiro (ESO) lenye makuu yake katika Wilaya hiyo.



Kwa mujibu wa mkuu huyo alisema bado wapo wazazi hadi leo wanawashawishi watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani ili wasifaulu ,


"mzazi unadiriki kumashawishi mtoto wako afanye vibaya kwenye mitihani ulimpeleka shuleni ya nn?kwakuogopa kuwa utakamatwa kwakuwa hukumpeleka mtoto shuleni" Alisema Batenga


Amesema kuwa Jambo Hilo linasikitisha Sana na lipo kwenye Jamii zetu hizi za kifugaji,hivyo amewaomba  kulifanyia jambo Hilo jilakufanyiwa kazi na kuchukua hatua kwa wazazi na walezi ambao wanawashawishi watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani na akifanya vizuri kwenye mitihani mtoto huyo anaenda kuadhibiwa.


"Serikali ya awamu ya sita haitavumilia vitendo vya namna hiyo kwasababu serikali inafanya kila juhudi inayowezekana kuboresha mazingira na miundombinu ya shule ili watoto wasome vizuri lakini baadhibya wazazi wanawapotosha watoto wafanye vibaya darasani "Alisema.


Kwa upande wake mbunge waJimbo Hilo Christopher Olesendeka alisemani kosa kubwa Sana kisheria ,serikali na sisis wawakilishi wa wananchi tutaungana na asasi hii ya (ESO) Kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi wetu ili kuhakikisha kwamba watoto wote wakike na wakiume watapewa fursa sawa ya kupelekwa shuleni na kumlinda mtoto wa kike apate elimu ,sio ya msingi tuu Bali Bali ya sekondari Pamoja ba ya vyuo vikuu..


 Olesendeka alisema Nia yetu ni kuwa na wasichana wa Jamii ya kifugaji ambao wao watakuwa na shahada zao moja au mbili au kwenda kwenye shahada ya uzamivu na wao waweze kutoa mchango kwa Taifa letu hata kwa familia wanazotoka hiyo ndiyo dhamira na Lengo tulilonalo kwa Jamii ya wafugaji .


Aliongeza kuwa wazazi wanaofanya hivyo wabadilike kifkra na kimtazamo waelewe dunia inaelekea wapi na mahitaji halali ya watoto wa kike.


Katibu mkuu wa shirika hilo  Lowasa Lormujey alisema kuwa kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni ili kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike katika kuhakikisha wanawake wawe katika mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo na kutimiza ndoto zao .


Lowasa alisema watoto wakike jamijbya wafugaji kipaumbele Cha wao kwenda shuleni hivyo kampeni ya niache NISOME ni sauti ambayo itawafanya mabinti hao watamani kusoma ili waweze kusimama na kufanikisha ndoto zao.


Ata hivyo mratibu huyo alisema shirika limelenga kuelimisha Jamii iki kuwasomesha ,kuwafuatilia na kuwasaidia watoto wa jinsia zoteili waweze kufikia ndoto zao kwa ustawi wa elimu ya Tanzania ,Pamoja na kutoa elimu kwa makundi yote ndani ya Jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa na jinsu ya kuepuka magojwa ya kuambukizw Ana yasiyo ambukiza ili kuwa najamii yenye afya katika Taifa na kuleta maendeleo ya Nchi yetu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI