Header Ads Widget

ELIMU YA UMILIKISHWAJI ARDHI KWA WANAWAKE YATOLEWA


Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake nchini Tanzania yameungana kwa pamoja kuadhimisha wiki ya mwanamke aishie Kijijini kwa kutembelea baadhi ya Mikoa ili kuelimisha haki ya mwanamke ya  kumiliki ardhi kwani imeonekana kuwa wanaume wamepewa kipaumbele kutokana na mfumo dume uliyopo katika jamii. Mwandishi wa Matikio Daima Rehema Abraham anaripoti toka Kilimanjaro

Aidha katika kuadhimisha siku hiyo  wadau hao wamelazimika kupita kwenye baadhi ya Mikoa hapa Nchini kwa ajili ya kutoa Elimu na kuhamasisha wanawake kufahamu haki zao katika umiliki wa ardhi na kuona ni changamoto zipi wanazokumbana nazo wakati wa kipindi hiki Cha ugonjwa wa UVIKO 19.

Mashirika hayo yalioungana ni pamoja na  chama cha wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) pamoja na Chama cha Haki Ardhi (LANDESA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto .

Akizungumza katika viwanja vya pasua mkoani hapa  Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amesema kuwa suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake mkoani Kilimanjaro Bado upo chini kutokana na mfumo dume wa wanaume kumiliki ardhi tofauti na mwanamke .

Mpogolo amesema miongoni mwa mikoa yenye changamoto juu ya kina mama kumiliki ardhi  Mkoa wa Kilimanjaro ni moja wapo na kusema inasababishwa na uchache wa ardhi hali ambayo hupelekea wanaume kumiliki  kuliko wanawake.

Bi.Fatma Kimwaga wakili na mratibu  kutoka Chama cha wanasheria  wanawake Tanzania TAWLA amesema kuwa katika kuadhimisha siku ya mwanamke wa Kijijini wamekuwa wakipokea malalamiko ya changamoto ya wanawake kutomiliki ardhi kwa sababu hawana fedha pamoja na mfumo dume ambao umekuwepo hapo nyuma.

"Katika jamii nyingi inaonekana kuwawanaume ndio anyepaswa kumilikina ardhi lakini pia kutokana na mfumo dume wanawake hao wameshindwa kumiliki ardhi kihalali lakini ukiangalia pia changamoto nyingine ambayo wanawake wanakutana nayo ni mume kufariki na ndugu wa Mume kun'gang'ania mali ikiwemo ardhi, na mwisho wa siku wanamtoa kwenye nyumba anakosa haki yake ya msingi"Alisema.Kimwaga,

Hata hivyo Katika utoaji wa elimu wameanza mkoa wa Mwanza, Misungwi, Babati na Arusha ambapo katika mikoa hiyo wameweza kuwaeleza umuhimu wa  mwanamke wa kijjijni anavyokuwa na thamani kubwa kwenye jamii hususani umilikishwaji wa ardhi na Kauli mbiu katika kuadhimisha siku ya mwanamke wa Kijijini ni" ARDHI NI NYENZO YA MAENDELEO KWA MWANAMKE WA KIJIJINI.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS