Header Ads Widget

TEHAMA NI NINI?

 

Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kuzagaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususani kompyuta na vitumi vyake. 

Kwa hali hiyo, maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha kuenea kwa lugha zinazotumika kwa wingi katika teknolojia hiyo kama vile Kiingereza na Kifaransa na kudumazwa kwa lugha za Kiafrika zinazotumiwa kwa nadra mno. Uwezo wa kutumia media na vitumi vipya vya teknolojia hii kwa ubunifu na uhakiki aghalabu hutegemea umilisi wake.


 Umilisi wa kidijitali nao ni zao la mafunzo kupitia lugha zoefu ambayo humpa mwanafunzi fursa ya kushiriki kikamilifu. Makala hii ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi mdogo uliofanywa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania kuonesha ufaafu wa Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia somo la TEHAMA katika shule za msingi. 

Matumizi ya Kiswahili kufundishia stadi za msingi za TEHAMA ni hatua ya mwanzo kuelekea kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili kutolea mafunzo ya kiufundi. Aidha, tunatathmini manufaa na changamoto zinazokabili matumizi ya Kiswahili kama lugha ya TEHAMA. 1.0 Utangulizi Ishara muhimu ya utandawazi ni ule uwezo wake wa kuyagusa maisha ya wanajamii wengi kwenye jamii anuwai katika nyanja za elimu, uchumi, siasa na utamaduni kwa jumla ambamo lugha hupata nafasi ya pekee.


 Lugha ni mfumo wa ishara nasibu za sauti wenye maana unaotumiwa na wanadamu katika mawasiliano baina yao.

 Ishara na taswira ambazo zinawakilishwa na kuwasilishwa na lugha huumba na kuathiri maarifa, stadi, mielekeo na tabia aijengayo mtu. Lengo la makala hii ni kuchunguza ufaafu wa Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia somo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shule za msingi nchini Tanzania.

 Makala hii ni zao la utafiti mdogo uliofanywa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, kusini mwa Tanzania. 

Tulitembelea shule za msingi za vijijini na kuwahoji walimu na wanafunzi wa madarasa ya 5, 6 na 7 kuhusu ufundishaji na ujifunzaji wa somo la TEHAMA kwa Kiswahili. 

Pamoja na kuhudhuria baadhi ya vipindi vya somo hili, watafitiwa waliulizwa maswali kama vile: Je, umilisi wa Kiswahili unawafaidisha vipi wanafunzi wa shule za msingi katika ujifunzaji wao wa somo la TEHAMA? Ni changamoto zipi zinazowakabili wanafunzi na walimu katika kujifunza na kufundisha somo la TEHAMA kwa kutumia Kiswahili? Je, kuna manufaa gani ya kutumia Kiswahili kufundishia somo la TEHAMA? TEHAMA ni somo lililoanzishwa katika mtalaa mpya wa Elimu ya Msingi (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, 2005).

 Somo hili linampa mwanafunzi maarifa na stadi za matumizi ya habari, vyombo vya mawasiliano na maktaba. 

Kwa hivyo, kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia somo la TEHAMA ni kukifanya kuwa nyenzo ya kuwasilishia elimu ya sayansi na teknolojia ya kisasa. Katika muktadha huu, madhumuni ni kuwasilisha stadi, mielekeo, na maarifa yaliyokusudiwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, ili lugha yoyote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS