Mbinga, Novemba 10, 2026.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Hamad Hassan Chande, ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Kanda ya Kusini, pamoja na taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara hiyo kwa juhudi za kukabiliana na migogoro kati ya wananchi na taasisi hizo, pamoja na kusimamia changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao ya kazi.
Pongezi hizo zimetolewa katika kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ambapo Naibu Waziri alikutana na watumishi wa Wizara hiyo kwa lengo la kupokea taarifa kuhusu hali ya migogoro na changamoto mbalimbali katika Kanda ya Kusini.
Katika kikao hicho, watumishi walimweleza Naibu Waziri hali halisi ya migogoro iliyopo, hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana nayo pamoja na maeneo yanayohitaji ufuatiliaji na ufumbuzi.
Aidha, kikao hicho kilitoa fursa kwa watumishi kueleza changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao, hususan usimamizi wa maeneo ya hifadhi na kuimarisha mahusiano kati ya wananchi na taasisi za Wizara.










0 Comments