Header Ads Widget

PROF. MKENDA AIPA DIT MAELEKEZO MAPYA KUIMARISHA UBUNIFU NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

 Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ameilekeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mafunzo ya ufundi na teknolojia, pamoja na kuhakikisha bunifu zinazozalishwa na taasisi hiyo zinafanyiwa biashara na kuingizwa sokoni ili kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumza kuhusu ziara ya Waziri huyo chuoni hapo leo novemba 10, 2026,  Makamu Mwenyekiti wa Baraza la DIT, Hanifa Mohamed, amesema Profesa Mkenda amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwaandaa vijana wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Amesema Waziri ameelekeza pia taasisi hiyo kutumia fursa za ushirikiano na vyuo vya kimataifa ili kuwawezesha wanafunzi kupata nafasi za masomo na ujuzi ambao haupatikani nchini, akitaja China, Uturuki na Moscow Urusi, huku akiwataka kutafuta fursa nyingine katika mataifa mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Marco Ndomba, amesema ziara ya Waziri Mkenda ilikuwa pia na lengo la kufuatilia maendeleo ya taasisi hiyo, ambapo amesisitiza umuhimu wa Tanzania kufikia hatua ya kujitegemea katika masuala ya ujuzi.

Amesema Profesa Mkenda ameielekeza DIT kubadili mwelekeo wa ubunifu kwa kuhakikisha bunifu zinazozalishwa haziishii kuoneshwa kwenye maonesho, bali zinafanyiwa kazi na kuingizwa sokoni kama bidhaa zinazoweza kutatua changamoto za wananchi.

Profesa Ndomba amesema taasisi hiyo imeahidi kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha bunifu hizo zinageuzwa kuwa bidhaa za kibiashara zitakazotumika na kuleta manufaa kwa jamii.

            








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI