Waratibu wa mafunzo ya faida ya Teknolojia katika afya na uchumi kutoka kampuni ya INKCYPUS & FAR FORLIFE katika picha ya pamoja na katibu wa mbunge jimbo la Ismani Mr Ndaso kushoto na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa wa Iringa Agrey Tonga wa pili kulia lengo kutumia fursa hiyo
NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa, Agrey Tonga, amekutana na kampuni ya teknolojia katika sekta ya afya na uchumi ya INKCYPUS & FAR FORLIFE, kwa lengo la kutafuta fursa za mafunzo na kuwawezesha vijana wa mkoa wa Iringa kunufaika na maarifa na teknolojia zinazoweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.
Tonga amefanya kikao hicho wakati kampuni hiyo ikiwa imeanza kutoa mafunzo ya bure kwa wananchi wa Iringa kuhusu matumizi ya teknolojia katika kuboresha fursa za kiuchumi pamoja na afya.
Katika hatua hiyo, Mwenyekiti huyo amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kushiriki katika programu mbalimbali zinazolenga kuwaongezea ujuzi, maarifa na uwezo wa kutumia teknolojia katika kujenga uchumi wao na jamii kwa ujumla.
Mkutano huo umefanyika leo katika viwanja vya CCM Mkoa wa Iringa, ambapo Tonga alikutana na waratibu wa mafunzo hayo, Lilian Maina na Alen Maturu, kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuwafikia vijana wengi zaidi wa mkoa wa Iringa.
Kwa upande wao, waratibu hao wameeleza kuwa mafunzo yanayotolewa na INKCYPUS & FAR FORLIFE yanalenga kuwafikia wananchi kwa kuwapatia elimu inayoweza kuwasaidia kutumia fursa za teknolojia katika masuala ya afya na maendeleo ya kiuchumi.
Kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kutoa nafasi kwa vijana kujifunza namna teknolojia inavyoweza kutumika kama nyenzo ya kujenga fursa mpya, kuongeza ufanisi katika shughuli zao na kutafuta njia mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.
Tonga amepongeza kampuni hiyo na kuwa magunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa vijana na kuwa atafanya mchakato ili UVCCM kupata mafunzo hayo .
Hata hivyo alisema serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imwendelea kuwakumbua vijana kupitia mikopo isiyo na riba pia miradi mbali mbali ukiwemo wa BBT hivyo UVCCM Iringa itashirikian na kampuni hiyo na wadau wengine wenye mipamgo ya kuinua vijana ili kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za ajira na uchumi kwa kutumia fursa zinazopatikana kupitia teknolojia.
Alisema ushirikiano kati ya UVCCM Iringa na kampuni zinazotoa mafunzo ya aina hiyo utasaidia kuongeza wigo wa vijana wanaofikiwa na programu za mafunzo, hususan wale wanaohitaji maarifa mapya katika kujenga shughuli zao za kiuchumi.






0 Comments