Morogoro
Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA SC) imeibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika mchezo wa mashindano ya SHIMMUTA-2026 uliochezwa asubuhi ya leo katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro.
Katika mchezo huo, TMDA SC ilianza kwa kasi, ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara yaliyowapa wapinzani wakati mgumu. Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 20, ambapo mshambuliaji wake Ramadhani Mohamed Chitunda aliifungia TMDA bao pekee la mchezo.
Baada ya kupata bao hilo, TMDA SC iliendelea kuimarisha mashambulizi huku ikidumisha nidhamu na uimara katika safu yake ya ulinzi hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Ushindi huo unaifanya TMDA SC kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa mashindano ya SHIMMUTA-2026.







0 Comments