Header Ads Widget

TAKUKURU YAMBANA MKANDARASI ALIYEKIMBIA NA FEDHA ZA MIRADI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa Kigoma imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 320 kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Gopa Constractors Tanzania Ltd aliyekuwa akitekeleza miradi ya soko la Kimataifa la Kagunga na jengo la Utawala la Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo alitoweka na fedha hizo na kuitelekeza miradi hiyo.


Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma, John Mgallah alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Kigoma akieleza utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha April hadi Septeemba mwaka huu katika uzuiaji na ufuatiliaji wa fedha za matumizi ya umma katika miradi.


Katika taarifa hiyo Mgallah alisema kuwa katika fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 260 kilirejeshwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kigoma lkutokana na mradi wa ujenzi wa soko la Kagunga mpakani mwa  Tanzania na Burundi na Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kwa mradi wa jengo la Utawala la halmashauri.


Mgallah alisema kuwa katika fedha walizorudisha kiasi cha shilingi milioni 60.4  kilirudishwa serikalini na shilingi 230,000 zilirejeshwa kwa wananchi na hivyo kuifanya taasisi hiyo kufanikiwa kurejesha kwa wahusika kiasi cha shilingi milioni 320.9


Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa Kigoma alisema kuwa awali Mkandarasi huyo alipewa malipo ya awali baada ya kuwasilisha nyaraka za benki lakini hakuonekana tena eneo la miradi na ndipo TAKUKURU walianza kazi ya kumtafuta na kufanikiwa kumkamata na kumrejesha mkoani Kigoma ambapo alikubali kurejesha fedha alizochukua.


Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari Mgallah alisema kuwa katika kipindi hicho TAKUKURU ilifanikiwa kufanya ufuatiliaji katika miradi 79 yenye thamani ya shilingi bilioni 36.5 na kwamba ufuatiliaji huo umeongeza elimu na umakini wa wananchi katika kusimamia na kutekeleza miradi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI