Na Matukio Daima Media, Kilosa
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa imeahidi kugharamia masomo ya kijana Inocent Mkuchu, ambaye ameacha chuo kutokana na ukosefu wa ada na kuamua kujishughulisha na ufugaji kabla ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo).
Ahadi hiyo imeolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba mjini Kilosa, baada ya kupata taarifa za changamoto iliyosababisha kijana huyo kushindwa kuendelea na masomo.
Shaka amesema ofisi yake itahakikisha gharama za masomo ya Inocent zinagharamiwa ili kumwezesha kurejea chuoni na kuendelea na elimu yake.
Uamuzi huo unampa kijana huyo fursa nyingine ya kuendeleza safari yake ya kielimu, huku ukisisitiza umuhimu wa kutambua na kusaidia vijana wanaokabiliwa na vikwazo vya kiuchumi katika kufikia ndoto zao.
Mwisho








0 Comments