Header Ads Widget

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE WASISITIZWA UMUHIMU WA USALAMA WA MITANDAONI.

 

Na, Jusline Marco;Arusha

Wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha kuwa vijana wanajua umuhimu wa usalama wa mitandaoni na namna ya kujilinda pindi wanapotumia mitandao ya kijamii.

Rai hiyo imetolewa na Mhadhiri mwandamizi wa chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, ambaye pia ni mbobezi wa masuala ya kompyuta na Mkurugenzi wa Shirika la COMTECH ALLIANCE, Dkt. Devotha Mnyambo wakati akizungumza katika maafali ya 3 ya kidato cha nne katika Shule ya sekondari ya Naurei Golden Soil iliyopo Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha.

Akizungumza katika maafali hayo amesema Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwenye uelewa, umakina na uchapishaji katika masuala ya usalama wa mitandaoni ambapo ameutaka uongozi wa shule hiyo kuangalia namna bora ya kuendelea kuboresha zaidi ya masomo ya sayansi ya kompyuta ambayo kwa sasa yameingizwa kwa kasi zaidi katika mitaala ya masomo nchini.

Aidha amesema  shirika la COMTECH ALLIANCE, Dkt. Devotha amesema shirika lilianzishwa kwa ajili ya kuweka uwiano kwa watoto wanaotoka katika familia za vijijini na walio kwenye maisha ya juu kidogo ili kutoa nafasi kwa watoto walio chini kujifunza nafasi za teknolojia za kidigitali pamoja na ubunifu wa Tehama.

Amesema ili kutimiza azma hiyo shirika hilo linafanya kazi katika shule mbalimbali za serikali pia na kutoa nafasi kwa shule za binafsi kwa ajili ya ushirika kupitia program mbalimbali zinazotolewa kwa vijana kujifunza mambo ya kidigitali sambamba na kubuni majawabu ya changamoto zinazoikumba jamii.

Mbali na kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwa na dira na maono ambayo yanamjenga kijana, Dkt. Devotha amesema nchi ya Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika  katika masuala ya usalama wa mitandaoni kwa umakina na uchapishaji.

Ameongeza kuwa uchumi wa nchi katika dira ya maendeleo 2050 ni uchumi wa kidigitali hivyo ameitaka jamii kujua masuala ya kidigitali na kuyapa kipaumbele ambapo pia ameutaka uongozi wa shule ya Naurei Golden Soil kuboresha eneo la teknolojia zinazoibukiabikiwa ni sambamba na Teknolojia ya akili unde(AI).

Sambamba na hayo amewataka wahitimu hao kujikita katika kujifunza masuala ya teknolojia ya kidigitali kutokana na maelekezo wa duniani kwa sasa kujikita katika matumizi ya teknolojia zaidi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nkoaruwa Bwn. Rejeaeli John Nko amempongeza Mkurugenzi wa shule hiyo kwa kuwa kilele cha elimu katika Kata ya Nkoaruwa kwa kuendelea kuunga mkono serikali katika kutoa elimu kwa jamii, ambapo ameahidi kama serikali kuendelea kushirikiana na wadau wote walio kwenye Kata hiyo kwaajili ya kukuza na kuendeleza elimu.


Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Bwn. Steven Ndosi amewataka wazazi na walezi kuona kuwa eneo pekee ambalo ni sahihi kuwekeze kwa ni elimu.


Mkuu wa Shule hiyo akizungumza katika maafali hayo ameendelea kuwasisitiza wanafunzi hao kuwa na nidhamu katika maisha yao kwani nidhamu ndiyo njia pekee ya kufanikiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI