Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
ZAIDI ya asilimia 70 ya kura za maoni alizopata Dkt. Netho Ndilito zimemuwezesha kupata uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Chamwino, katika mchakato uliowakutanisha wagombea 34.
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi na kamati za chama kuanzia ngazi ya kata, wilaya hadi mkoa, akisema ushirikiano wao ulikuwa sehemu ya safari yake ya kuwania uteuzi ndani ya chama.
Aidha, amewataka wagombea wenzake walioshiriki katika mchakato wa kura za maoni kuweka pamoja nguvu zao na kufanya kazi kwa ushirikiano, akisisitiza umuhimu wa mshikamano kuelekea uchaguzi ujao.
Dkt. Ndilito amesema kwa sasa anatarajia kukamilisha hatua zinazofuata kwa kujaza na kurejesha fomu kwa kuzingatia maelekezo ya chama. Pia, amewahimiza wananchi wa Chamwino kujitokeza kuunga mkono CCM pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao.








0 Comments