NA HADIJA OMARY ,MATUKIO DAIMA MEDIA,LINDI.
Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso, amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Emirates Builders Company Ltd kuhakikisha ndani ya wiki mbili mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Nachingwea unaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Gharama za Mradi huo ni shillingi 2, 587,672,026.00 na unaotakiwa kihudumia watu wapatao 45,000 wa wilaya hiyo ya Nachigwea ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 90
Waziri Aweso ametoa agizo hilo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika Kijiji cha Mkumba, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wananchi wa Nachingwea wanaanza kunufaika na huduma hiyo kwa wakati.
Agizo hilo la Waziri Aweso limetolewa mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mhe. Fadhili Liwaka, kulalamikia uhaba wa maji safi na salama jimboni humo na kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hiyo.
Mbunge Liwaka amesema wananchi wengi wa Jimbo la Nachingwea bado wanakabiliwa na adha ya ukosefu wa maji licha ya jitihada zinazoendelea.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji (MANAWASA) Kiula Kingu
Maradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni moja (1,000,000) kwa siku na utakapokamilika utasaidia kuongeza uwezo wa vyanzo vya maji katika mji wa Nachingwea na kupunguza changamoto ya ukosefu wa maji iliyopo sasa.
Amesema Mradi unatarajia kuhudumia watu wapatao 45,000 walioko Nachingwea mjini ikiwemo stesheni, Hospitali camp, majengo, Calfonia, Ugogoni Mkumba shamba na Nangoe
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Nachingwea wamemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassani kwa kuwajengea mradi huo mkubwa wa miundombinu ya maji ambao unaenda kupunguzaa adha ya shida kubwa ya maji katika wilaya yao.









0 Comments