Header Ads Widget

WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI YA KIFUSI MGODI WA KITAITA,GAIRO

 

Na Matukio Daima Media, Morogoro 

Watu watano wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika duara la uchimbaji wa madini kwenye mgodi wa Kitaita, wilayani Gairo mkoani Morogoro.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhar Kubecha, zimeelezs kuwa watu tisa waliingia kwenye duara hilo kinyemela majira ya usiku kwa ajili ya shughuli za uchimbaji.


Kubecha amesema watu hao, ambao hutambulika kwa jina la “wadudu”, walipatwa na ajali hiyo baada ya kifusi kuwaangukia wakiwa ndani ya duara.

Amesema miili ya watu watano imepatikana, ambapo mwili mmoja tayari umetambuliwa kuwa ni wa mkazi wa Kilindi.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, taarifa za awali zinaonyesha kuwa baadhi ya marehemu wanatoka nje ya Wilaya ya Gairo.

Mwisho

MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SKA2026 TUNAOMBA KURA YAKO WAWEZA KUPIGA KURA KIRAHISI KULIKO KUPITIA LINK HII⬇️⬇️⬇️

KUPIGA KURA BONYEZA HAPA


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI