UONGOZI wa Nuru FM Iringa kwa kushirikiana na familia ya mwanahabari Frank Vegulla umetoa taarifa kuhusu hali yake ya afya, ukieleza kuwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya kuugua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 5, 2026, Vegulla ambaye ni miongoni mwa wafanyakazi wa Nuru FM, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Wodi Namba 10, ambako anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
Uongozi huo umeeleza kuwa ndugu, jamaa na watu wengine wanaohitaji kupata taarifa sahihi na za moja kwa moja kuhusu maendeleo ya afya yake wanashauriwa kuwasiliana na ndugu yake, Johnson Vegulla, kupitia namba ya simu 0763 499 579.
Aidha, familia imeeleza kuwa watu watakaoguswa na hali ya Frank na kutamani kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kumsaidia katika kipindi hiki wanaweza kufanya hivyo kupitia M-Pesa Lipa Namba 353280515, jina likiwa Johnson Vegulla.
Familia na uongozi wa Nuru FM wamewashukuru ndugu, marafiki, wafanyakazi wenzao pamoja na wadau mbalimbali kwa upendo, mshikamano na moyo wa kujitolea wanaoendelea kuuonesha katika kipindi hiki.
Pia wameendelea kuwaomba wananchi na wasikilizaji wa Nuru FM kumuombea Vegulla ili apate nafuu na kurejea katika hali yake ya kawaida.
Matukio Daima Media tunamuombea Frank Vegulla apate nafuu na kupona haraka.
KUPIGA KURA ZA SAMIA KALAMU AWARDS KWA MATUKIO DAIMA MEDIA INGIA HAPA






0 Comments