Header Ads Widget

TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA USAFIRI ENDELEVU, NOVEMBA


Na Matukio Daima Media

Tanzania inatarajia kuadhimisha Siku ya Usafiri Endelevu Novemba mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya usafiri salama, rafiki kwa mazingira na unaozingatia mahitaji ya jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya wahariri na waandishi wa habari,katika mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Dk Habibu Suluo, amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 4 hadi 6 mwaka huu.

Amesema Novemba 6 itakuwa siku ya kilele cha maadhimisho hayo, ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri watakutana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli zitakazoandaliwa.

Kwa mujibu wa Suluo, wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki katika maadhimisho hayo, yakiwemo maonesho yatakayohusu sekta ya usafiri.

Amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wananchi kupata taarifa na elimu kuhusu sekta ya usafiri, pamoja na kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hilo.

Aidha, amesema kauli mbiu inayotarajiwa kutumika katika maadhimisho hayo inalenga kuhamasisha usafiri endelevu, salama na rafiki kwa mazingira, huku ukichangia maendeleo ya jamii.

Maadhimisho hayo pia yatatumika kutoa taarifa kuhusu shughuli mbalimbali za sekta ya usafiri, ikiwemo usafiri wa anga, pamoja na kutoa nafasi kwa wadau kujadili maendeleo ya sekta hiyo.

Suluo amewataka wadau wote kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho na shughuli nyingine zitakazoandaliwa wakati wa maadhimisho hayo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI