Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUZINDUA MAJENGO, BARABARA MTUMBA DODOMA.

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 8, 2026 anatarajiwa kuzindua majengo ya Ofisi za Wizara 26, Taasisi za Serikali 11 pamoja na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1 katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo ndani ya Mji wa Serikali Mtumba, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya utendaji wa Serikali jijini Dodoma.


Kabudi amesema majengo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya ujenzi wa Mji wa Serikali, ambayo ilianza Oktoba 2021 baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa majengo 23 ya muda.


Amesema awamu ya kwanza ilianza Novemba 28, 2018 na kukamilika Machi 22, 2019, huku ikiambatana na ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na jengo la TARURA.


Kwa mujibu wa Waziri huyo amsema, awamu ya pili imejikita katika ujenzi wa majengo ya kudumu ya wizara na taasisi za Serikali pamoja na miundombinu muhimu inayowezesha eneo hilo kufanya kazi kama mji wa kisasa.


Amesema miongoni mwa miundombinu iliyokamilishwa ni barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1, mfumo wa umeme wa chini ya ardhi wenye urefu wa kilomita 42, maji safi na maji taka, mawasiliano pamoja na miundombinu ya TEHAMA.


Kabudi amesema pia zimejengwa kamera za ulinzi, kituo cha zimamoto, miundombinu ya kukabiliana na majanga, huku mazingira yakiboreshwa kupitia upandaji miti na uwekaji wa mandhari ya kisasa.


" Uwanja wa Mashujaa nao umekamilishwa na umejumuishwa katika miundombinu itakayozinduliwa, hatua inayolenga kuongeza matumizi ya eneo hilo kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, " Amesema.


Ameeleza kuwa ujenzi wa Mji wa Serikali umezingatia dhana ya mji janja na mji wa kijani, ikiwamo matumizi ya nishati jadidifu, uvunaji wa maji ya mvua, mipango miji na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Kabudi amesema majengo hayo yamejengwa kwa kuzingatia mahitaji tofauti ya wizara na taasisi, yakiwa na uwezo wa kuchukua watumishi 300, 500, 1,400 na takribani 150 kwa jengo, kulingana na muundo uliotumika.

" Baada ya kukamilika kwa majengo hayo, yatawezesha watumishi 18,510 kutekeleza majukumu yao ndani ya Mji wa Serikali Mtumba, huku Serikali ikiwa imeandaa samani kwa ajili ya Wizara 26 na Taasisi 11," Amesema .


Na Kuongeza  "Utekelezaji wa mradi huo umehusisha wakandarasi 11, ambapo watano ni taasisi za Serikali na sita ni kampuni za sekta binafsi, huku usimamizi wa usanifu na ushauri ukifanywa na taasisi tano za Serikali, " Amesema.


Kwa upande wa miundombinu, Kabudi amesema TARURA imehusika na barabara, DUWASA maji na maji taka, TANESCO umeme, TTCL mawasiliano, TEMESA kamera za ulinzi na e-GA miundombinu ya TEHAMA.


Amesema TPDC imehusika na miundombinu ya gesi asilia, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika vituo vya zimamoto, huku TFS ikihusika na upandaji miti na uboreshaji wa mandhari ya eneo hilo.


Waziri Kabudi amesema kukamilika kwa Mji wa Serikali kutarahisisha usafiri na upatikanaji wa huduma, huku miundombinu hiyo ikitarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo ya Mtumba, Mahoma Nyika, Ihumwa, Chamwino, Dodoma Mjini, UDOM na Hombolo.

Mwisho

KUPIGA KURA ZA SKA MATUKIO DAIMA INGIA HAPA  


MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026 ILI KUSHINDA TUZO HIZO INAHITAJIKA KURA ZA WANANCHI ZA KUTOSHA HIVYO TUNAOMBA KURA YAKO KUPIGA KURA BONYEZA LINK HII CHINI KISHA UTAONA SEHEMU IMEANDIKWA KURA KURA UTABONYEZA NA MWISHO SEHEMU IMEANDIKWA NDIO UTAKUWA UMEPIGA KURA UTAFANYA HIVYO KWA TUZO YA KWANZA HADI YA NNE.

⬇️⬇️⬇️BONYEZA HAPA 
KUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ISHINDE TUZO ZA SKA 2026 INGIA HAPA KIRAHISI ZAIDI
 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI