Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo akikagua nyumba ambayo mtuhumiwa alijificha baada ya kuwaona polisi
Baba wa mtuhumiwa aliyeuawa
Na Matukio Daima Media, Kilosa
TUKIO la kutekwa kwa mwanamke na mtoto wake katika Kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro limeishia kwa kifo cha Kokan State (30), baada ya mwanaume huyo kudhibitiwa kwa risasi na polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, Kokan alikuwa akitafutwa kwa tuhuma zinazohusisha mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia silaha.
Kantimbo akasema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu ambapo baada ya kubaini alipo na kumfuata, alimshika mwanamke aliyekuwa alimhudumia kinywaji pamoja na mtoto wake mdogo na kujifungia nao katika chumba, akiwatumia kama kinga dhidi ya polisi.
Alisema Kokan alitishia kuwaua Mama na mtoto huyo kwa sime iwapo polisi wangejaribu kumkamata, hali iliyosababisha askari kutumia silaha na kumuua baada ya jitihada zote za kutaka ajisalimishe kushindikana.
Mwanamke na mtoto waliotumiwa kama Kinga na mtuhumiwa wa uhalifu
Mwanamke huyo aliyetekwa, mkazi wa Kijiji cha Parakuyo, Rehema Masuke, amesema tukio hilo liliwapa hali ya hofu wakiamini huenda wangeuawa kwa sime aliyokuwa nayo kijana huyo.
Kwa upande wake Baba mzazi wa Kokan amesema kwa muda mrefu alikuwa akimkanya mwanawe kuacha kujihusisha na Matukio ya ki uhalifu, lakini licha ya ushauri huo, alihusishwa mara kadhaa na matukio hayo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Parakuyo, Emmanuel Kibasisi, amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na uhalifu.
Polisi mkoani Morogoro wameendelea kutoa wito kwa vijana kujiepusha na uhalifu na kutafuta kipato kupitia shughuli halali.
Mwisho
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA
MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA
PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM
PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
3:TUZO YA AFYA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
4:TUZO YA MPIGA PICHA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .











0 Comments