Header Ads Widget

MWANAMFALME EDWARD RUKIDI KIJANANGOMA KUTAWAZWA KUWA MFALME WA TOORO SEPTEMBA 29


Mwanamfalme Edward Rukidi Kijanangoma, ambaye hivi karibuni alitangazwa kuwa mfalme mpyaUfalme wa Tooro magharibi mwa Uganda, anatarajiwa kutawazwa rasmi Septemba 29, 2026.

Hatua hiyo inafuatia kuidhinishwa kwake na Baraza Kuu la Kifalme la Tooro baada ya kutambulishwa kama mrithi wa marehemu Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV.

Hata hivyo, uteuzi wake umeibua mvutano ndani ya familia ya kifalme kuhusu suala la urithi wa kiti cha enzi. Baadhi ya wanafamilia wa karibu wa marehemu mfalme, akiwemo mama yake na dada yake, wamepinga uamuzi huo.

Wanaopinga uteuzi huo wanadai kuwa mtoto wa marehemu mfalme ndiye anayestahili kurithi ufalme huo kwa mujibu wa wosia wa marehemu. Hata hivyo, mtoto huyo anayehusishwa na madai hayo hajawahi kutambulishwa rasmi mbele ya taasisi za ufalme.

Mvutano huo umeendelea hata baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda kuripotiwa kuishauri serikali kuzingatia matakwa ya wosia wa marehemu mfalme katika mchakato wa kumpata mrithi. Lakini viongozi wa ukoo wa kifalme walikataa msimamo huo, wakisisitiza kuwa masuala ya urithi wa ufalme yanapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia taratibu na mila za ufalme, si kwa maelekezo ya serikali.

Licha ya upinzani huo, viongozi wa ukoo wa kifalme wameendelea na maandalizi ya sherehe ya kutawazwa kwa Prince Edward kama ilivyopangwa.

Wakati huohuo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, amemuunga mkono hadharani Prince Edward Rukidi Kijanangoma, akimtaja kuwa mrithi halali wa marehemu Mfalme Oyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI