Header Ads Widget

MUFTI AWATAKA MASHEKHE WA MIKOA KUANZISHA MIRADI YA KIUCHUMI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally amewataka viongozi na waumini wa dini ya kiislam nchini kutumia mafundisho ya dini kuwa kichocheo katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya mandeleo ya kiuchumi ya wananchi ambapo amewataka mashekhe wa mikoa nchini kote  kusimamia jambo hilo.

Mufti Zubeir amesema hayo Septemba 17 katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kidini ya siku mbili mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa viongozi wa dini na waumini wao kuwa kwa viongozi na waumini wa kiislam kuwa na  miradi ya kiuchumi kunawaondoa kwenye suala la kuwa ombaomba na kuchochea kila mmoja kufanya kazi.

Akizungumza katika uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma Mufti zubeir alisema kuwa  Baraza Kuu la Waislam linaitambua baadhi ya mikoa  vitovu kwa ajili ya mafundisho ya dini mkoa Kigoma ukiwa mmoja wapo hivyo ni lazima dini ifundishe vijana na waumini wake kuishi kwa maadili mema ya kutukuza Mungu, kuheshimu viongozi lakini pia dini inafundisha waumini wake namna ya kutawanyika katika uso wa dunia kwa ajili ya kutafuta riziki za kila siku maana yake ikiwa kufanya kazi.

Awali Mufti Zuberi alifika ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma ambapo alipata bahati ya kufanya kikao kidogo na Kaimu Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk.Rashid Chuachua ambaye alimweleza kuwa mkoa Kigoma uko shwari na ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma inashirikiana vizuri na viongozi wa dini katika masuala ya dini na kutekeleza mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa alisema kuwa viongozi wa dini mkoani humo wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta Amani na kuufanya mkoa huo kuwa na maendeleo na ndiyo maana katika uchaguzi mkuu uliopita hakukuwa na vurugu zozote kutokana na wagombea, wapiga kura na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuzingatia misingi ya dini zao katika kuepuka suala la k

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI