Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi amezindua msikiti mkubwa wa Ijumaa katika mji mdogo wa Nguruka (Masjid Nuru) ambapo ametaka viongozi wa dini kutumia misikiti na madrasa kufundisha maadili na tabia njema kwa jamii.
Mufti Zuberi alisema kuwa mafundisho ya dini yanapaswa kuwa maisha ya kila siku ya Watanzania katika kuzingatia maadili, kutii viongozi, kusaidia jamii na kuwaongoza katika ucha Mungu.
Alisema kuwa kwa kuanzia lazima vijana wadogo wapelekwe madrasa ili kufundishwa dini, kujifunza mambo ya hija na hata anapokuwa mtu mzima na kupewa mamlaka na madaraka atawatendea mema watu anaowangoza.
Pamoja na hilo Mufti Zuberi ameonya waumini wa kiislam kuwa maakini na matumizi ya teknolojia ya akili Mnemba (AI) katika kufuatialia mafundisho ya dini kwenye mitandao ya Computer kwani mafundisho mengine yanapotosha na kwenda kinyume na mafundisho ya dini na Hadithi za Mtume Muhamada (SAW).
Akizundua msikiti huyo Shekhe Mkuu alisema kuwa wameuteua msikiti huo kuwa moja yaa misiki ya Kitaifa ambao utakuwa unasimamia na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) na kwanza uongozi wa Msikiti huo utateuliwa na Shekhe Mkuu na baraza laake badala yaa kufanya uchaguzi wa kuongoza msikiti huo kutokana na mambo na sifa ambazo msikiti huo inazo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mfadhili wa ujenzi wa Msikiti huo, Kailima Ramadhani ambaye ni Mkurugenzi wa Tume Huru ya uchaguzi Tanzania (INEC) alisemaa kuwa amejtolea kusaidia ujenzi wa msikiti huo kutokana na hali aliyoona misikiti ya eneo hilo ambapo aliweza dhamira ya mamabo matatu ikiwemo ujenzi wa Msikiti na madras ya kufundisha dini na masomo mbalimbali ya kiislam.
Mhandisi wa mradi huo, Seif Hamisi huyo alisema kuwa msikiti huo wenye uwezo wa kuchukua waumini 300 kwa wakati mmoja utKuwa na vyumba viwili vya madrasa kwa ajili ya kufundisha dini, eneo la kutawadhia sambaamba na ujenzi wa vyoo vyaa matundu 10, chumbaa cha kuoshea maiti,ofisi ya Imam wa Msikiti, vyumba viwili vya Maktaba,kisima chenye urefu wa mita 150 , matanki mawili ya kuhifadhia maji na vituo sita vya kugawa maji kwa wananchi wa eneo hilo ambayo yatatolewa bure huku kukiwa na taa 12 za Mwanga wa jua zilizojengwa kuzunguka eneo la msikiti.









0 Comments