Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji wa kurekebisha mifupa kwa njia ya kunyoosha na kurefusha kwa wagonjwa wenye ulemavu wa mifupa inayojulikana kama Ilizarov technique.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa, Dkt. Dismas Cosmas, amesema kuwa upasuaji huo unaowezesha kurekebisha na kunyoosha mifupa kwa kutumia mbinu hiyo ya kisasa ambapo huduma hiyo inalenga kusaidia wenye ulemavu wa mifupa unaotokana na majeraha au ajali, pamoja na wagonjwa wenye hali za ulemavu wa mifupa walizozaliwa nazo, hususan watoto.
Upasuaji huo umefanyika kwa kushirikina na Taasisi ya Orthocycle Foundation kutoka Manchester, Uingereza, pamoja na Taasisi ya Watanzania Wauguzi wanaoishi Uingereza (TUHEDA United Kingdom).
Aidha, Dkt. Cosmas amewashukuru wataalam hao pamoja na taasisi hizo kwa kufanikisha zoezi hilo na kueleza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuimarisha huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa nchini.










0 Comments