WAFANYABIASHARA na wajasiliamali zaidi ya 500 kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu zinatarajia kushiriki maonyesho ya kimataifa ya biashara ya ukanda wa ziwa Tanganyika yatakayoanza mkoani Kigoma kuanzia Septemba 16 mwaka huu.
Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu maonyesho
hayo yanayojulikana kama Lake Tanganyika Internationa Expo 2026 alisema kuwa maonysho hayo ni muendelezo wa mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa Kimkakati kwa uchumi na biashara.
Balozi Simon Sirro alisema kuwa Maonyesho yatafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 22 Septemba mwaka huu kwenye uwanja wa Community Centre na Waziri wa viwanda na Biashara, Judith Kapinga atafungua rasmi maonyesho hayo Septemba 18 mwaka huu.
Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa maonyesho hayo ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa mkoa Kigoma na mikoa mbalimbali nchini kutangaza biashara zao kulingana na soko lililopo nchi za maziwa makuu lakini pia kubadilisha uzoefu wa teknolojia na namna ya wafanyabiashara watakavyoweza kutengeneza muunganiko wa kufanya biashara kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Akizungumza katika mkutano huo Meneja wa Chemba ya Taifa ya biashara (TNCC) mkoa Kigoma , Prosper Guga alisema kuwa mwitikio kwa wafanyabiashara wanaotaka kushiriki maonyesho hayo ni mkubwa ukilinganisha na idadi ya wafanyabiashara 500 ambao chemba ilikusudia na sasa idadi ni kubwa Zaidi ya hiyo.
Guga alisema kuwa kwa mfano Chemba ya biashara ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imethibitisha kuwa na wafanyabiashara 200 ambao watakuja kwenye maonyesho hayo wakiwemo wachimba madini kutoka majimbo mbalimbali ya nchi hiyo ukilinganisha na idadi ya washiriki 50 waliyopewa awali.
Mwisho.









0 Comments