Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam
WAZIRI MKUU Mstaafu na Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, ameanguka ghafla na kupoteza fahamu wakati akihutubia mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini, ulioandaliwa na kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Tukio hilo limetokea leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakati Jaji Warioba akiendelea kutoa hotuba yake mbele ya washiriki wa mkutano huo.
Baada ya kuanguka, Jaji Warioba alipewa msaada na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kutafakari hali ya kisiasa nchini, pamoja na masuala yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa Tanzania.
Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu hali yake ya kiafya bado hazijatolewa rasmi.







0 Comments