Header Ads Widget

CCM YAFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WA MIKOA 32

 




Na Matukio Daima Media

DAR ES SALAAM: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya kiutendaji katika ngazi ya mikoa kwa kuwateua Makatibu wapya wa CCM katika mikoa yote 32 ya kichama nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Labani Kihongosi, Septemba 27, 2026, mabadiliko hayo yamefanyika kwa lengo la kuimarisha utendaji wa chama katika ngazi za mikoa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Makatibu hao wapya wameanza majukumu yao mara moja, huku CCM ikieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya chama na ufuatiliaji wa shughuli zake katika maeneo mbalimbali.

Aidha, Katibu Mkuu wa CCM, Asha-Rose Migiro, ametangaza kufanyika kwa Semina Elekezi ya siku mbili kwa viongozi hao, itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 29 hadi 30, 2026.

Kwa mujibu wa CCM, semina hiyo inalenga kuwajengea uwezo viongozi hao pamoja na kuwaandaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao mapya kwa ufanisi.

Katika taarifa hiyo, CCM imewashukuru Makatibu wa CCM wa mikoa waliomaliza muda wao kwa utumishi na mchango wao katika kukijenga chama, huku ikisisitiza kuwa itaendelea kutumia uzoefu na uwezo wao kama sehemu ya hazina ya viongozi na watendaji wa chama.

Miongoni mwa Makatibu wapya waliotajwa ni Pilly John Jackson kwa Mkoa wa Arusha na Stanley Wilson Mkandawire kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI