Wauguzi 17 kutoka hospitali mbalimbali za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani leo wamehitimu mafunzo ya vitendo ya Uuguzi wa Msingi katika Huduma za Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (Hands-on Critical Care Nursing), yaliyolenga kuimarisha ujuzi wao katika kutoa huduma salama na bora kwa wagonjwa mahututi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Ukunga na Uuguzi wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utasishaji, Bi. Aneth Kaduma, amesema mafunzo hayo yamewajengea wauguzi uwezo wa kutumia kanuni za huduma kwa wagonjwa mahututi, pamoja na kutambua na kudhibiti mapema hali zinazohatarisha maisha ili kuboresha matokeo ya matibabu.
Baadhi ya wahitimu wamesema watatumia ujuzi walioupata kuboresha huduma za uuguzi katika vituo vyao na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora, salama na kwa wakati.










0 Comments