Na Mwandishi wetu
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala mbali mbali ya kisiasa na Kijamii,Luqman Maloto,amewapa ushauri Dk.Emanuel Nchimbi,Makamu wa Rais na Dk Mwigulu Nchemba,Waziri Mkuu wa Tanzania,juu ya kutumia nafasi zao kusaidia maendeleo ya nchi, badala ya kutumia nafasi hizo kujipanga kwa ajili ya Urais wa 2030.
Katika andiko lake aliloipa jina la ’SAUTI ZA MTAA KUHUSU, NCHIMB, NCHEMBA NA URAIS’ Malotoa ameandika kuwa Hakuna mahali popote, sauti ya Nchimbi imewahi kurekodiwa au kunukuliwa kwamba anajiandaa kwa urais Uchaguzi Mkuu 2030. Kadhalika Nchemba, hakuna alipopata kusema, Hata hivyo, mitaani wanazungumzwa kuwa shabaha yao ni kumrithi Rais Samia.
Katika andiko hilo ameeleza kuwa katika meza ya Rais Samia Suluhu Hassan ina vitendawili vingi vya kutegua huku kadhia ya Oktoba 29, 2025 ikichukua nafasi kubwa kwenye ubongo pmaoja na uwepo wa Tume tatu sasa ikiwemo inayoohusisha majaji kutoka nje ya nchi na kwamba lipo jambo zito linatafutwa,majibu yake yapatikane ili hatua zichukuliwe na nchi iwe salama.
Aidha andiko hilo la Maloto limeeleza kuwa mbali na hayo katika Meza ya Rais Samia kuna suala lake na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kujenga uwekezaji mkubwa wa nishati Afrika Mashariki.
Ziarani yake Angola kwa mwaliko wa Rais Joao Lourenço “J-Lo”, kuzindua Hospitali ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere ikiwa ni ziara ya faraja na Fahari ya kenzi jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Maloto katika andiko lake hilo ameainisha masuala mengi yanayofanywa na Rais Samia Kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi miongoni mwa hayo ni pamoja na kuwapokea marais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo. William Ruto (Kenya) na Paul Kagame (Rwanda), kisha Ruto aliyehutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Pamoja na kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin kisha kurejea kuwa mwenyeji wa mkutano wa ushirikiano wa kujenga na kuboresha miundombinu kwa nchi washikadau Afrika, Africa50 General Shareholders.
Ameeleza kuwa ni muhtsari wa mengi na Rais Samia ana wasaidizi wawili wakuu kikatiba; Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi, na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba licha ya kuwa Kwa muundo wa Serikali, Rais Samia ana wasaidizi wengi, lakini wakuu ni hao wawili ambao Utendaji wao na namna ambavyo wanamsaidia kazi Rais Samia, vipimo vyake anavyo yeye Mwenyewe Rais
Hata hivyo Maloto mbali ya kusema vipimo vya namna wanavyomsaidia Rais, pia ameweka wazi Sauti za wananchi aliyoipa jina Sauti za mtaani kuhusu Nchimbi na Nchemba licha ya kuwa hawajatangaza popote kuwania Urais lakini wanatajwa kutokana na mienendo yao kuonyesha utayari wa kumrithi Rais Samia.
“Kwa nini wanasemwa hivyo? Isijekuwa Nchemba anahukumiwa kwa historia ya mwaka 2015. Naam, Nchemba aligombea tiketi ya CCM, katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho. Nchimbi hakushiriki mchakato mwaka 2015. Sasa kwa nini atajwe leo?”ameandika Maloto huku akieleza kuwa Walezi wa Kiswahili walioshi miaka dahari iliyopita, walipata kusema “lisemwalo lipo”.
” Nchemba na Nchimbi waliwanong’oneza watu wao wa karibu, nao wakavujisha? “Hakuna siri ya watu wawili”, ni ngano nyingine ya wahenga.
Ameongeza kuwa ama wanasingiziwa au ni kweli wanajipanga kimyakimya, mitaa inazungumza kuwa Nchimbi na Nchemba wanaukodolea macho urais 2030, na kwamba kila mmoja anachanga karata zake ipasavyo.
”Iwe ni kweli taarifa zao wanazivujisha kwa makusudi, au zinavujishwa kwa dhamira mbaya, ukweli wa mtaani ni huo.”ameandika Maloto na kuhoji
”Je, Nchimbi na Nchemba wana ndoto ya urais au wana tamaa ya kuupata? Tuanze hapa; kuna tofauti kubwa kati ya ndoto na tamaa.
Mwenye kuota huwa na subira, huamini wakati wake sahihi utafika. Aliyejawa tamaa, huona zamu yake inachelewa.”
Katika eneo hilo Maloto ameeleza kuwa hapo ndipo kwenye elimu ya msingi; kwamba mtu mwenye tamaa ya urais, hata akiwa sehemu ya serikali yenye Rais mwingine, hufanya mambo kwa ajili ya kujisafishia njia kwenda Ikulu kuliko kuitumikia nchi inavyopasa, kutokana na ile nafasi aliyopo.
Ameongeza kuwa Wasaidizi wa Rais wenye tamaa ya urais ni sumu. Hawakawii kuvujisha hata siri za wenzao kwa lengo la kuharibiana.
” Tunakumbuka jinsi watu walivyoshughulikiana nyakati za mwisho wa urais wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi, vita ikawa kubwa kuelekea kumrithi Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, vivyo hivyo wakati wa kumpokea kijiti Rais wa Nne, Jakaya Kikwete.”ameandika Maloto.
Amesema Rais akiwa na msaidizi mwenye tamaa ya urais, hawezi kuwa na uaminifu wa kuitetea serikali. Machoni kwa rais anaweza kutoa kila aina ya sifa, pembeni atamponda kiongozi wake kwamba hawezi kazi.
Na atahakikisha anajitenga na lawama za Serikali, wakati yeye ni sehemu yake.
”Kipo kiburi hujengeka kwa mwenye kuusaka urais. Kwanza huanzisha makundi, halafu hujiona yeye ndiye anayeweza kazi kuliko hata aliyepo madarakani. Na kwa kawaida huwezi kumwongoza mtu anayejiona ana uwezo mkubwa kuliko wewe.”ameandika Maloto na kuwaachia Swali Nchimbi na Nchemba kama ni kweli wanaukodolea macho urais, je, wao wana ndoto au wana tamaa na cheo hicho? Na kama Wanaweza kukubali kupokea risasi kuitetea Serikali wanayoitumikia? Kwamba ni Vema kukaa pembeni ili kutumikia ndoto, kuliko kumsaidia Rais kwa ujanjaujanja.
Katika andiko lake hilo amewapa Ushauri kuwa Uongozi huletwa na Mungu, japo jitihada hazikatazwi na kutolea mfano wa Rais wa 38 wa Marekani, Gerald Ford,kuwa hakugombea urais, wala hakuwahi kusimama kama mgombea mwenza.
Maloto amesema hata hivyo, Ford aliteuliwa kisha kupitishwa na Baraza la Wawakilishi kuwa Makamu wa Rais, baada ya aliyekuwepo, Spiro Agnew, kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi.
Katika mifano mbali mbali aliyoitoa Maloto katika andiko lake hilo amesisistiza Wasaidizi wa Rais wafanye kazi
Wamsadie Rais Samia kuwaletea maendeleo Watanzania.
”Urais kama umepangwa na aliye juu, wataupata. Wafanye kazi kwa ajili ya kulisaidia taifa. Pengine utendaji wao ndiyo ukawabeba. Siyo kujaza makundi na kusababisha serikali itawaliwe na sarakasi.
“Wasaidizi wa Rais wafanye kazi badala ya kuutolea macho urais. Tamaa ya urais itawafanya wawe wapinzani wa Rais Samia, sasa watawezaje kufanya kazi kwa maelewano ili kuwaletea Watanzania maendeleo? Msaidizi mwenye tamaa ya urais, hutamani Rais afeli ili yeye apate mtaji wa kisiasa.”amehitimisha andiko lake Maloto
Mwisho






0 Comments