Header Ads Widget

RC SENDIGA: TUWAPE UMMA TAARIFA SAHIHI ZA DAWA NA VIFAA TIBA


Na: Mwandishi wa Matukio Daima Media, Babati.


MANYARA - Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuzingatia sheria na maadili ya taaluma wakati wa kuripoti masuala ya dawa na vifaa tiba.

Amesema hayo leo Agosti 20, 2026 alipofungua rasmi kikao kazi cha wahariri wa habari kutoka Kanda ya Kaskazini kilichoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini, TMDA, katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Babati.

RC Sendiga ameipongeza TMDA kwa kuwa mstari wa mbele kulinda afya za jamii tangu kuanzishwa kwake na kusema mkutano huo ni hatua muhimu ya kuhakikisha umma unapata taarifa sahihi.

"TMDA imeonesha dhamira ya kweli kuhabarisha umma kuhusu dawa na vifaa tiba. Mkutano huu na Wahariri ni mustakabali sahihi na naamini mkitoka hapa mtaenda kutoa taarifa sahihi kwa jamii," amesema.

Aidha, amewataka wananchi na watumishi wa serikali kutoa taarifa kwa TMDA na mamlaka nyingine za usalama iwapo watakutana na dawa au vifaa tiba bandia na duni. 

"Niwapongeze wanahabari kuhabarisha umma. Tuzingatie mipaka na sheria za nchi kwani hakuna uhuru ambao hauna mipaka. Rai yangu kwa wahariri na wanahabari tusisitize maadili ya taaluma zetu," amebainisha.

RC Sendiga pia amewakaribisha wawekezaji Mkoa wa Manyara kwa kuwa ni miongoni mwa mikoa inayokua kwa kasi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Dawa za Binadamu na Mifugo wa TMDA, Dkt. Yona Mwalwisi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dkt. Adam Fimbo, amesema mamlaka hiyo inaendelea kushikilia cheti cha ISO 9001:2015 na ithibati ya maabara ISO 17025:2017, uthibitisho wa ubora wa huduma zake. 

Katika kikao hicho mada 8 ziliwasilishwa zinazohusu udhibiti wa bidhaa duni na bandia.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI