Header Ads Widget

WANANCHI WAZIDI KUFURIKA BANDA LA MUHIMBILI KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2026

 


Mamia ya wananchi wameendelea kufurika katika Banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ili kupata huduma mbalimbali za afya, elimu na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa hospitali hiyo.

Wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kujionea huduma za kisasa za kibingwa na kibingwa bobezi zinazotolewa na Muhimbili, ikiwemo elimu ya huduma za dharura, uchunguzi wa awali wa afya, ushauri wa kitaalamu pamoja na maonesho ya teknolojia zinazotumika katika utoaji wa huduma za upasuaji.

Baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo wamesema wamevutiwa na namna Muhimbili ilivyowasogezea huduma karibu, hatua iliyowawezesha kupata elimu sahihi ya afya na kuelewa kwa undani zaidi huduma mbalimbali zinazopatikana katika hospitali hiyo ya taifa.

Kutokana na mwitikio huo mkubwa, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeendelea kuwakaribisha wananchi kutumia siku zilizobakia za maonesho kutembelea banda hilo ili kupata elimu ya afya, ushauri wa kitaalamu na kujionea ubingwa na ubobezi unaotolewa na hospitali hiyo katika kuimarisha afya na kuokoa maisha ya Watanzania.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI