![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti akipata maelezo ya Vitabu vya Kiada vilivyofanyiwa maboresho ya Mitaala ya Elimu kwenye banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). |
Na. Mwandishi Wetu, Dar.
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti ameipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa namna ilivyofanya maboresho ya Mitaala ya Elimu nchini yenye lengo la kumfanya muhitimu kuweza kujiajiri au kuajiriwa mara anapomaliza masomo yake.
Mhe. Magoti ameyasema hayo leo tarehe 12/7/2026 katika maonesho ya Sabasaba ambapo amesema kuwa TET inafanya kazi nzuri ya kuboresha elimu nchini.
"Kwa kweli nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuboresha Elimu nchini hasa hivi karibuni katika maboresho ya mitaala yaliyofanyika, ni tumaini langu kwamba wanafunzi nchi nzima wataendelea kufanya vyema, " Amesema mhe. Magoti.
Pia ameeleza, anafurahia namna wanafunzi wanaendelea kupatiwa vitendea kazi kama vitabu vinavyowapelekea kuendele kufanya vyema wakati wa masomo yao na kuendelea kuipongeza TET kwa uratibu mzuri na upatikanaji wa vitabu mashuleni.
TET inashiriki katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba yaliyoanza tarehe 28, Juni ambapo yanatarajiwa kufungwa hapo kesho, Julai 13.
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti akipata maelezo kwa Vitabu vya Kiada vilivyofanyiwa maboresho ya Mitaala ya Elimu kwenye banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). |








0 Comments