MARKO PHILIMON CHUMA
Simu: 0777939139
S.L.P. 616
Tarehe: 10 Julai, 2026
Kwa:
Mheshimiwa Waziri,
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,
S.L.P. 3151,
Dodoma.
YAH: BARUA YA SHUKRANI KWA KUPA UZITO NA KULIFANYIA KAZI OMBI LETU LA DHARURA KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA ALIOFANYIWA DADA YETU
Mheshimiwa Waziri,
Kwa heshima na taadhima kubwa, naomba nikushukuru kwa dhati kwa namna ulivyolipokea na kulipa uzito ombi letu la dharura kuhusu dada yetu, Tumwimbie Chuma, mkazi wa Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa.
Kupitia hatua ulizochukua baada ya kupokea barua yetu, umetupa matumaini makubwa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kusimamia haki, kulinda utu wa wananchi wake na kusikiliza kilio cha wanyonge bila ubaguzi. Jambo hili limetugusa sana na limetupa moyo mkubwa.
Mheshimiwa Waziri, uongozi wako umeonyesha mfano wa uadilifu, uwajibikaji na huruma kwa wananchi. Kitendo cha kulipokea ombi letu na kulifuatilia kwa uzito kinaonyesha wazi kuwa Wizara yako ipo karibu na wananchi na inatimiza wajibu wake wa kulinda wanawake na makundi maalum dhidi ya vitendo vya ukatili.
Kwa niaba ya familia yetu, tunakushukuru kwa dhati kwa kutusikiliza na kwa kuonyesha kwamba sauti ya mwananchi wa kawaida ina thamani mbele ya Serikali. Hatua hii imetupa imani ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa taarifa za matukio yanayohitaji uingiliaji wa haraka ili haki itendeke na maisha ya wananchi yaendelee kuwa salama.
Aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Media za Matukio kwa ushirikiano, sapoti na nafasi waliyoitoa katika kuibeba sauti yetu. Mchango wao umeifanya jamii kutambua kilio cha familia yetu na umetupa faraja kwamba bado wapo watu na taasisi zinazojali haki za wananchi. Mwenyezi Mungu awabariki sana, awaongezee hekima, ujasiri na mafanikio katika kazi yao ya kuhabarisha umma na kutetea maslahi ya wanyonge.
Tunakuombea Mwenyezi Mungu akupe afya njema, hekima, busara na nguvu za kuendelea kulitumikia Taifa letu kwa uadilifu na weledi. Tunaamini kuwa chini ya uongozi wako, wananchi wengi zaidi wataendelea kupata haki na msaada wanaouhitaji.
Kwa mara nyingine, tunasema ahsante sana Mheshimiwa Waziri, na ahsanteni sana Media za Matukio Daima chini ya mkurugenzi wake na mwanahabari nguli Francis Godwin kwa kusimama nasi katika kipindi hiki kigumu.
Mungu awabariki mno na azidi kuwalinda katika majukumu yenu ya kila siku pia kuendelea kuwapambania kwa kuwasemea watanzania wanaonyanyaswa.
Naomba kuwasilisha.
MARKO PHILIMON CHUMA






0 Comments