Header Ads Widget

WAAJIRI SEKTA BINAFSI KILWA WAKUMBUSHWA KUZINGATIA USTAWI WA WAFANYAKAZI

           


                                                                                                                 

Waajiri wa sekta binafsi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, wamekumbushwa umuhimu wa kuzingatia kikamilifu miongozo ya Serikali kuhusu ustawi wa wafanyakazi ili kuhakikisha ajira wanazotoa zinawawezesha watumishi kujikimu kimaisha.


Wito huo umetolewa na Katibu Tarafa wa Pwani, Mfaume Sudi, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo, wakati wa mafunzo maalum yaliyojikita katika sheria za kazi na marekebisho yake. Mafunzo hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Afisa Kazi wa Mkoa wa Lindi na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Akizungumza katika mafunzo hayo, Sudi aliwataka waajiri kutambua umuhimu wa kusajili taasisi na kampuni zao katika NSSF pamoja na kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kuhakikisha wanapata stahiki zao za hifadhi ya jamii.



Kwa upande wake, Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi, Juma Namuna, alieleza haki na wajibu wa waajiri wa sekta binafsi kwa mfuko huo, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu za hifadhi ya jamii.


Naye Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Idara ya Kazi na Ajira Mkoa wa Lindi, Nisata Bureta, alisema sekta binafsi zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi.



Aidha, Afisa Kazi Mkoa wa Lindi, Festo Boyi, alisisitiza umuhimu wa waajiri wa sekta binafsi kuzingatia kima cha chini cha mshahara kilichowekwa na Serikali ili kulinda maslahi ya wafanyakazi.


Baadhi ya waajiri walioshiriki mafunzo hayo walieleza kuwa kikao hicho kimekuwa na tija kubwa kwao, huku wakibainisha maeneo mbalimbali yanayohitaji maboresho ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa sheria za kazi na hifadhi ya jamii.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI