Header Ads Widget

DKT. KIJAJI ATETA NA WAZIRI WA CHINA KUHUSU USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA UTALII

 


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Utamaduni na Utalii wa China Mhe. Gao Zheng katika Mkutano wa 126 wa Baraza Tendaji la Shirika la Utalii Duniani uliofanyika nchini Teledo, Hispania.


Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano wa diplomasia ya uchumi hususani katika Sekta ya Utalii kati ya Tanzania na China.


Viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu mikakati ya kuvutia watalii, kukuza uwekezaji, na kubadilishana uzoefu na matumizi ya teknolojia katika utalii.


Aidha katika kikao hicho, Dkt. Kijaji alibainisha kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana kwa karibu na China ili kukuza Sekta  ya Utalii baina ya nchi hizo mbili, huku akieleza kuwa China ni moja ya soko muhimu la utalii na la kimkakati kwa Tanzania.  



Aidha, alibainisha umuhimu wa kuendeleza programu za mafunzo na kubadilishana utaalamu ili kuhakikisha kuwa pande zote zinanufaika kutokana na fursa zilizopo.


Pande zote mbili zilikubaliana kuendeleza mazungumzo hayo na kuanzisha hatua za utekelezaji wa ushirikiano zaidi, ikiwemo miradi ya pamoja ya utalii, uwekezaji wa kimkakati, na kampeni za kukuza bidhaa za utalii zinazovutia soko la kimataifa. 


Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza idadi ya watalii, kuongeza mapato ya utalii, na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na China.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI